Tuesday, January 18, 2011

                                                KIMBIA
Hakuna mtu ambaye kristo alimuokoa ,akamtoa katika uovu aliokua nao kisha akamuingiza katika himaya  yake(Kanisani) ili afie(aozee) kanisani. Bali lengo kubwa la kristo ni kumfanya mtu huyo aongeze nguvu katika kuujenga mwili wa kristo

            Afikapo kanisani Kristo humpa Neema mtu huyo kutambua nafasi yake kiutendaji kama ni mwalimu,muimbaji,mchungaji n.k. Baada ya hatua ya kujitambua Kristo kupitia Roho Mt (Yoh14:26) ambaye ni mwalimu huanza kutufundisha namna ya kutumika katika eneo hilo kwa ustadi wa hali ya juu. Bidii ya mtu katika kujifunza chini ya Mwl Mkuu Roho Mt hutupeleka viwango mpaka viwango kiutendaji.

           Hivyo haina ubishi kuwa viwango alivyonavyo mtumishi yeyote ni matunda ya namna ambavyo alimtii au anamtii mwalimu wake mkuu ambaye ni Roho Mt. Hapa haijalishi mtu ameokoka lini kwa kuwa uaminifu na kufaulu  chini ya huyu mwalimu ndio hutuhamisha darasa hadi darasa, ndiyomaana si ajabu ukakuta mtu hatoki katika darasa alilonao miaka na miaka.

MUNGU huja na kupima kazi ya kila mtu kwa kadri alivyowekeza ndani ya mtu huyo
                                                                                 
         Mtazamo au kiu ya Kristo baada ya kutuokoa anataka aone KAZI tuzifanyazo tuwapo katika himaya yake. Bidii maarifa na ustadi wa uchezaji wa kila mmoja alie katika mwili huu ndio hitaji lake la ndani. Kwa kua hukumu ya mtakatifu(aliyeitwa) ni juu ya kazi anazozifanya kwa ajili ya Kristo awapo chini ya jua na suala la dhambi Kristo alishamalizana nalo alipoangikwa Golgota.

        Kumbuka MUNGU ni zaidi ya Mchumi,anapowekeza hatarajii kupata hasara, kila sekunde hutaka kuona faida ya uwekezaji wake ndani yetu.Toka anatuokoa aliwekeza kwetu kwa namna kuu tatu
      a)Alitutoa katika mikono ya yule mwovu
      b)Akatuingiza katika Furaha ya pendo lake
      c) Anatufundisha kila uchao namna ya kutembea nae na namna ya kutumia hazina(vipawa) vilivyo ndani    yetu


Baada ya kuwekeza kwa gharama zote hizo yeye hukaa pembeni na kuangalia utendaji wa kila raslimali zake (watu wake) kwa kadri alivyo wekeza, ndio maana kwenye akasema 1kor 3:13-14(yeye atakuja kupima kazi ya kila mmoja). Biblia inataja kazi/matendo mema alizofanya Tabitha“Doricas” Mdo 9:36 na MUNGU alipoziangalia akarudisha uhai wake kupitia Petro. Nabii “Mikaya” yeye alisimamia kile ambacho MUNGU alisema na kamwe hakupindisha hata aliposimama mbele ya mfalme. Na hii ni mifano michache ya kazi baba zetu waliotutangulia.
 
Askofu Moses Kulola mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo ametumia uwezo wa KIMUNGU ulio ndani yake kuutangaza ufalme wa MUNGU katika maisha yake yote
 
Ili kumpenzeza MUNGU hatuna budi kila aliye kwenye mwili wa kristo  afanye kazi katika eneo lake(mraba) kwa nguvu, kwa kua mwekezaji hupita nakuangalia faida peke yake kwa kuwa hasara haipo kwenye mikakati yake, ndomana mlegevu(asiyezaa) hutupwa nje. Ajapopita huja na kuzipima kazi zetu kwa moto. Je ya kwangu ijapopita katika moto wa kristo itatoka kama dhahabu au itateketea kama majani makavu? Hilo ni swali la kujiuliza kisha KIMBIA na kufanya kazi ya MUNGU kwa nguvu zako zote na kwa kadri ya hazina aliowekeza ndani yako.
                                                                                

By Victor N. Mboya                                                                

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...