Groove Awards ni tuzo kubwa za muziki wa injili nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla. Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya sita sio tu zinahusisha kazi za wanamuziki wa Injili nchini humo bali hujumuisha pia kategori ya wanamuziki wa injili toka kila nchi zilizo Afrika mashariki na kati ambao nyimbo zao zinafanya vizuri nchini Kenya. Mwaka huu tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Tarehe 30/04/2011 kuanzia saa Saba mchana katika ukumbi wa Kenya International Conference Centre (KICC) na kuonyeshwa LIVE na Television ya NTV.
Kabla ya tuzo hizo washiriki watapata fursa ya kufaya tour katika miji ya Nakuru, Mombasa, na Machakos. Katika kategori ya waimbaji wa injili toka Tanzania wanaofanya vizuri nchini kenya waliochagulia ni
ARTIST OF THE YEAR (TANZANIA)
26a. Bahati Bukuku
26b. Bonnie Mwaitege
26c. Christina Shusho
26d. Neema Mwaipopo
26e. Rose Muhando
26f. Upendo Nkone
No comments:
Post a Comment