Thursday, April 21, 2011

Kanisa lafanyia IBADA kwenye Nightclub

Phase II Night club ni ukumbi maarufu wa disko ulio katika jiji la Kensas nchini Marekani ambapo watu mbalimbali hukutana kwa ajili ya kustarehe katika siku za ijumaa na jumamosi usiku.Kwa hali ya kawaida huwezi amini kuwa panaweza kutumika kama kanisa ambapo watu huja na kumsifu Mungu. Tofauti na ilivyozoeleka ukumbi hutumika kama  mahali pakufanyia ibada kuanzia saa kila jumapili saa Tano asubuhi mpaka saa saba na nusu mchana.

Mchungaji Marvin Kirkwood
Mchungaji Marvin Kirkwood  ni mchungaji ambaye hufanyia ibada zake katika ukumbi huo. Mch Kirkwood amekuwa mshirika wa kanisa la Memorial Baptist Church lililo katika jiji la Kensas kwa Takribani miaka 15 akitumika kanisani hapo kama Mchungaji wa Vijana kwa kipindi cha miaka nane(8) na sasa anatumikia wito wake kwa Bwana chini ya huduma yake iitwayo Contagious Revival Church of Kansas City.

Akijibu swali kwanini ameamua kutumia Nightclub kama kanisa, Mch Kirkwood alisema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa anataka kuwafikia watu ambao injili kwao ni nadra kuwakuta kwa namna ya kawaida na lengo lake sio kuwapelekea dini ya ukristo bali kuwafikishia habari njema za Kristo zilizojaa upendo wa Mungu. Amesema yeye sio Mchungaji wa kawaida kama walifanyavyo wengine wahubirio maneno yaliyopangiliwa ili kuhadaa watu.

Mch Kirkwood  anaendesha ibada kama kawaida ikiwa ni pamoja na kuhubiri Neno la Mungu, kwaya, na vikundi vya kusifu na kuabudu

Angalia kwa makini clip ifuatayo na umsikilize Mch Kirkwood kuhusu huduma yake.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...