Friday, April 29, 2011

Mtazamo wa waislamu dhidi ya Serikali ya Tanzania


Mh Mrisho Jakaya Kikwete
Kwa siku za hivi karibuni ndugu zetu waislamu wamekuwa wakiandaa makongamano mbalimbali nchini. Moja kati ya maazimio ya makongamano hayo ni kufanya harakati ili kutokomeza mfumo Kristo unaoitawala Tanzania kwa miaka mingi. Katika siku za hivi karibuni limefanyika kongamano la waislamu katika mji wa Morogoro baada ya lile lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee.

 Lengo la kuyaweka maazimio ya kongamano hilo ni kuwawezesha  wakristo nao kujua nini ndugu zetu wanawaza juu ya nchi hii. Ikumbukwe wengi wa wakristo  wamekuwa na maisha ya pembe tatu yaani Nyumbani Kazini/mashuleni  -- kanisani  na kutokana na ratiba hizo pamoja na sababu nyingi wanashindwa kupata habari mbalimbali.

Baadhi ya Vipengele vilivyomo katika tamko la waislamu mkoani Morogoro lililotolewa katika msikiti mkuu wa Boma Road mjini humo ni kama ifuatavyo.

a)Kutaka liundwe Bunge la katiba tofauti na hili la sasa wanalodai lina wakristo wengi kuliko waislamu. Pia wanaitaka Serikali ilivunje baraza la mitihani nchini Tanzania (Necta) kwa madai kuwa lililopo lina wakristo wengi, hivyo kushindwa kuzingatia haki na maslahi yao.Pamoja na hayo wanaitaka serikali ipige marufuku uwepo wa mabucha ya Nguruwe kwenye maeneo yenye waislamu wengi.

b)Wameitaka serikali kurejesha kwa waislamu shule na taasisi zote za waislamu zilizotaifishwa na serikali enzi za Mwl J.k Nyerere ikiwemo shule ya Uhuru iliyoko katika mji wa Morogoro.

c)Wameunga mkono maamuzi ya Kongamano la waislamu lililofanyika jijini Dar es salaam lililopinga kwa nguvu zote jitihada za kuuzima uislamu nchini kupitia  mkutano uliofanyika siku za nyuma jijini Dr es salaam katika hoteli ya Moven Peak kati ya Maaskofu na Masheikh. Wamedai katika mkutano huo uliohudhuriwa na masheikh kadhaa, waislamu wa Tanzania hawapaswi kuunga mkono mapendekezo ya mkutano huo kwa kuwa masheikh wote walioshiriki ni Masheikh njaa wasioutakia mema uislamu na waislamu wa Tanzania.

d)Hawatakuwa tayari kuikubali katiba mpya itakayoundwa hapa nchini endapo haitokuwa na kipengele cha kuutetea uislamu na waislamu wa Tanzania kupitia vyombo muhimu kama mahakama ya kadhi pamoja na jumuiya ya waislamu OIC.


Aidha moja kati ya watoa mada katika kongmano hilo sheikh Illunga Hassan alisema  moja kati ya mambo yanayodhihirisha serikali ya Tanzania imetawaliwa na mfumo Kristo ni siku ya Ibada. Alisema serikali imeitambua siku ya jumapili na jumamosi kama siku za ibada kwa wakristo kupumzika, wakati ijumaa siku ya waislamu kuabudu haitambuliwi kama siku ya kuabudu ilihali waislamu ni wengi nchi hii kuliko wasabato ambao huabudu jumamosi.

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...