Jumapili ya jana katika jiji la Nairobi, zilifanyika tuzo za muziki wa Injili nchini Kenya. Katika tuzo hizo ambazo wanamuziki wapya waliibuka kidedea dhidi ya wanamuziki wenye majina makubwa. Mwanamama Christina Shusho alifanikiwa kunyakua tuzo ya Mwanamuziki Bora toka nchini Tanzania huku Rose Mhando akinyakua tuzo ya the Best Ringtone of the year.
Katika hali iliyoonyesha upendo na kuthamini kazi ya wenzake, Mwanamuziki Daddy Owen anayetamba na nyimbo yake ya SALUTE,alipopewa tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume nchini kenya aliamua kumkabidhi Julianni. Julianni ambaye hufanya Gospel Hiphop ni maarufu sana hasa kwa vijana nchini humo. Kwa waliobahatika kuona au kusikiliza nyimbo za Julianni, watakubaliana na Hosanna Inc kuwa ili nyimbo hizo ziwe gumzo nchini Tanzania zinahitaji miaka ya kutosha kutokana na mentality ya kanisa la Tanzania.
Paul Mwai akitoa shukrani zake mara baada ya kufanikiwa kuchukua tuzo mbili,ya Album bora ya Mwaka na Nyimbo bora ya kuabudu ya mwaka |
Rose Muhando akisema jambo mara baada ya kuchukua tuzo ya Mwanamuziki bora toka nchini Tanzania kwa niaba ya Christina Shusho ambaye hakuwepo ukumbini hapo. |
No comments:
Post a Comment