Friday, April 29, 2011

Groove Awards 2011 kufanyika Jumapili Ijayo


Groove Awards ni tuzo kubwa za muziki wa injili nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla. Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya sita sio tu zinahusisha kazi za wanamuziki wa Injili nchini humo bali hujumuisha pia kategori ya wanamuziki wa injili toka kila nchi zilizo Afrika mashariki na kati ambao nyimbo zao zinafanya vizuri nchini Kenya. Mwaka huu tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Tarehe 30/04/2011 kuanzia saa Saba mchana katika ukumbi wa Kenya International Conference Centre (KICC) na kuonyeshwa LIVE na Television ya NTV.




Kabla ya tuzo hizo washiriki watapata fursa ya kufaya tour katika miji ya Nakuru, Mombasa, na Machakos. Katika kategori ya waimbaji wa injili toka Tanzania wanaofanya vizuri nchini kenya  waliochagulia ni

ARTIST OF THE YEAR (TANZANIA)
 26a. Bahati Bukuku
 26b. Bonnie Mwaitege
 26c. Christina Shusho
 26d. Neema Mwaipopo
 26e. Rose Muhando
 26f. Upendo Nkone

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...