Wednesday, April 13, 2011

Je mtu aliyeokoa anaweza kuwa na mapepo?

Babu kulola akifanya maombezi katika moja ya mikutano yake ya injili
Pamoja na uzuri wa maisha ya wokovu ambao kwa Damu ya thamani kristo alitupatia bure, ni makosa makubwa kukaa na kufikiri kuwa mtu akiiisha kuokoa hawezi kabisa kwa njia yeyote kuingiwa na mapepo.

Katika (Mathayo 10:1-3 na Yohana 13:27) Tunaona pamoja na Yuda kutembea na kristo, lakini aliweza kutumika na upande wa Pili(giza) ilikufanikisha kazi za shetani. Pamoja na kuokoka mtu aliyeokoa anaweza kumpa shetani nafasi  ikiwa ataingia katika kufanya mambo yafuatayo.

a)  Kuruhusu uwoga na hofu imtawale 2Timotheo 1:7 na 1Yoh 4:18, kuwa na hofu ni  mwanya mkubwa unaotumiwa na ibilisi, ni ishara tosha kuwa mwenye hofu haamini uweza wa Mungu juu ya jambo husika, hivyo ile hali ya kuzubaa kwa Mungu haupo asilimia mia moja huku mazingira yanakua na Nguvu kuliko Neno la Mungu huu ni mwanya tosha wa ibilisi kuingia na kufanya atakavyo. Uwoga ulipomuingia Petro alishindwa kuendelea kutembea juu ya maji(Mathayo 14:27).

b)   Hali ya kuwa na mashaka kuona kuwa shetani na vikosi vyake anaweza kutudhuru muda wowote. Yakobo 1: 6-7  Hali hii inapokaa kwa muda mrefu ndani ya mtu wa Mungu hupelekea saa zote kumuona shetani na si Mungu. Kwake wokovu unakuwa sio udhihirisho wa nguvu za Mungu tena bali unabaki kama utaratibu wa kawaida(litrugia) mithili ya dini kama dini nyingine. Kwenye maombi na mafundisho atahudhuria lakini hii hali hubaki pale pale endapo hatoitambua.Ni rahisi kuona ni sehemu ya maisha kwa kua ndio amezoea lakini sio sahihi. Wakati mwingine watu wa aina hii huwa hawataki kumshirikisha mtu hali wanayopitia katika maisha yao ya kiroho, na pindi nguvu za giza zinapowaingia bado wanakua hawajitambui huku wakiendelea kwenda ibadani na kufanya vitu vyote kama wapendwa. Hii ni kwa kuwa maisha waliokuwa wakiishi kabla ya mapepo kuingia na baada ya mapepo kuingia yanautofauti kidooogo sana, hivyo kwa mhusika ni vigumu kuitambua hiyo hali ilihali watumishi wanaomzungua wenye ufahamu huligundua hilo.

 
c)   Mikataba na maagano ya kipepo iliyowahi kuwekwa kabla ya kuamua kuokoka.Biblia inasema Tazama mtu akiwa ndani ya Kristo amekua kiumbe kipya, yakale yamepita tazama yamekuwa mapya. Hii inamaanisha pamoja na kuwepo maaagano huko nyuma kabla ya kuokoka,baada ya kuokoka mtu huyu anakuwa kiumbe kipya, hutolewa katika giza na kuwekwa nuruni, Hivyo asipopata mafundisho yakutosha hujikuta anawakati mgumu kwa kuwa kule alikotoka na alikokuwa na ulinzi mkubwa wa kipepo kutokana na maagano yaliyokuwepo hayuko tena na huku kwa kristo hana misingi imara hivyo ni rahisi kuvamiwa na mapepo.Ni kama mtu aliyeachiwa kutoka gerezani kisha akaanza kuishi uraiani huku akivaa mavazi ya gerezani. Mtu wa namna hii maagano yote ya kipepo yanapaswa kuvunjwa kwa gharama kubwa zaidi kuliko ile ya awali iliyowekwa ili kuyabatilisha maagano yaliyowekwa hapo awali Matendo 19:18-19.

Ili kukabiliana na hayo,yatupasa kama wakristo kuifahamu kweli ya Neno la Mungu na kuishi katika hiyo Yoh 8:31-32. Pili  Kuishi kwa kumtazama kristo pasipo uwoga,wasiwasi au mashaka pasipo dhambi kwa kuwa dhambi humpa ibilisi nafasi ya kututesa tena Yoh 5:11-14. Tatu kuvunja mikataba yote ya kipepo iliyowahi wekwa kabla ya kuokoka
 

3 comments:

  1. mtu aliye okoka hawezi kuingiliwa na mapepo kwa sababu nikinyume chaneno la Mungu.Yuda alikua destined kufanya kile alicho kifanya na wakati huo alipoingiliwa na Ibilisi bado Kristo alikua ajamaliza mission yake iliyomleta Duniani Yani wokovu na upatanisho baina ya Mungu na Binadamu.Ndio maana alisema imekwisha shetani hana nafasi katika watoto wa Mungu..ndio maana tunaye Roho mtakatifu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yangu leo hii tunawatu wengi tu wapo makanisani lakini wanamapepo.
      Mwandishi ametaja mlango wa pepo kuwa ni hofu\woga
      Bado watu wapo makanisani lakini wana hofu iliyopitiliza
      Ayubu 3:25

      Delete
  2. MWALIMU.CHAMBUA MDUMAJune 2, 2012 at 9:38 AM

    MTU ALIYE OKOKA ANAWEZA KUINGILIWA NA MAPAPO ENDAPO ATALETA MCHEZO BAADA YA KUOKOKA.UKISOMA KITABU CHA LUKA NENO LINASEMA PEPO ANAKUJA NA KUCHUNGULIA NYUMBA YAKE YA ZAMANI NA AKIONA IPOIPO TU HUENDA NA KUCHUKUA PEPO WENGINE WABAYA KULIKO YEYE NA KUMVAMIA MTU HUYU.LAKINI MTU AKISIMAMA VIZURI NA YESU HAWEZI PEPO KUPATA NAFASI JUU YA MTU HUYU.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...