Tuesday, August 2, 2011

Jifunze kupitia Historia ya kundi la Sowers Group


Sowers Group kutoka kushoto ni Oswald, Mike, Kotso pamoja na Christeline (mke wa Mike)
Sowers ni kundi maarufu sana la muziki wa injili Afrika mashariki na kati. Historia ya kundi hili lenye jumla ya wanamuziki wanne, waatu wa kiume na mwanadada mmoja, inaanzia nchini Kongo Kinshasa zamani Zaire ambapo vijana watatu waliokuwa wakiishi pamoja ambao ni Mike Matumaini , Oswald Basoka na Kosto Zahinda waliamua kuondoka katika mji wa Bukavu waliokuwa wakiishi kuelekea jiji la Kinshansa kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyopelekea kutoweka kwa amani mjini Bukavu.

Wakati wakikimbia machafuko hayo siku ya tatu wakitembea kwa miguu kwa zaidi ya Kilometa 600 walijikuta mikononi mwa Askari jeshi mwenye bunduki ambaye aliwaweka kizuizini. Cha kushangaza pamoja na kwamba askari huyo alikuwa amewakamata wao na watu wengine aliamua kuwaachia watu wote na kuwashikilia vijana hao.

Sowers Group
Mungu aliwaokoa na mkono wa askari huyo ndipo safari ikaendelea, wakiwa Kinshasa machafuko tena yalitokea hali iliyowalazimu wakimbilie katika nchi ya Rwanda kwa usalama zaidi. Wakiwa nchini Rwanda Mike na Oswald ambao ni ndugu wakiwa na rafiki yao wa toka utotoni Kosto walikuwa wakiimba kama njia ya kuwafariji wenzao ambao walikuwa wamekata tamaa.

Katika kipindi hicho,ndipo  ambapo Kundi hili lilianza kuota mizizi kiuimbaji, liliungana na Christerine Mugeni binti mwenyeji wa Rwanda aliyeolewa na kijana Mike wa Sowers na kufanya kundi hilo kuwa na memba wanne na sio watatu kama ilivyokuwa hapo awali.

Wakiwa nchini Rwanda kundi lilizidi kukua kiuimbaji na kiroho huku likihudumu katika kanisa moja dogo lililoko jijini Kigali nchini humo. Kipindi chote hicho hawakuwa na jina ambalo walilitumia kama utambulisho wa kundi hilo,ndipo siku moja walipokuwa kwenye maombi Mungu aliwapa jina hilo la SOWERS GROUP.

Sowers wakiimba kwenye Tamasha la SAUTI ZA BUSARA mjini Zanzibar 2010
Nyimbo zao za kwanza kabisa katika album yao ya kwanza iliyoitwa 7x70 Umva na Jerusaleem, zilipata kibali kwa Mungu hususani Umva na kuvifanya vituo kadhaa vya Radio katika nchi hiyo kupiga nyimbo hiyo asubuhi wakati wa kufungua Redio na jioni wakati wa kufunga Redio.


Mwanadada Christeline mke wa Mike, yeye alijiunga rasmi na SOWERS mara baada ya kumalizika kwa album yao ya kwanza. Baada ya kutoa album hiyo ya kwanza kudi hilo lilipata Neema ya kwenda nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya mafundisho ya Muziki iliyochukua takribani miezi kumi na nane (18).


Baada ya kutoka nchini Uganda kundi hilo lilo lilihamishia makazi yake mkoani Arusha nchini Tanzania. Wakiwa nchini Tanzania Sowers walifanikiwa Kuzindua Album yao waliyoipa jina la Cheza(Dance)

Kwa sasa kundi zima la sowers liko nchini Australia katika jiji la Sydney. Mike wa Sowers ameiambia Hosanna Inc kuwa wako nchini humo ki huduma na wamefanikiwa kufanya huduma sehemu mbali mbali nchini humo.

Sowers wakiimba nchini Australia
Sowers ni kundi la kwanza la muziki wa injili lenye makazi yake Afrika Mashariki linaloongoza katika kupata nafasi za kwenda kuhudumu sehemu mbalimbali duniani. Wakiwa nchini Australia mnamo tarehe 22may 2011, Sowers walifanikiwa kuperfom katika moja ya matamasha makubwa nchini humo liitwalo Central Cost Show.
Mike na Chriteline wakiwa na familia yao pamoja na wana Sowers Oswald na Kosto
Licha ya kuimba, vijana hawa wanauwezo mkubwa wa kutengeneza nyimbo zao wenyewe kuanzia audio mpaka video. Walipokuwa nchini miezi kadhaa iliyopita walikuwa bize wakitengeneza video ya nyimbo zao mpya walizoimba wakishirikiana na Upendo Kilahiro.

The Sowers wakiimba kwenye Tamasha la Muziki wa Injili katika chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)


Sowers wakifanya Interview na Kituo cha Redio cha ABC FM nchini Australia

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...