Katika mwezi uliopita hapa Hosanna Inc tulikuwa na Swali lililosema
Watumishi wa Mungu wengi hawapendi kujihusisha na mchakato wa kupata katiba mpya?, hali hii inatokana na
1. Kutojua umuhimu wake
2. Kutoijua katiba yenyewe
3. Kuwa Bize na huduma
Kulingana na kura za wengi ni kwamba wengi wamesema tatizo la watumishi kutojihusisha na mchakato wa kupata katiba mpya kunatokana na “Kutojua Umuhimu wa katiba” . Hivyo ni changamoto kwa Kanisa kuijua katiba yetu kwa kina ili tuwe na upeo mpana wa kushiriki katika zoezi Hilo.
Swali la Mwezi huu kama lionekanavyo juu upande wakulia mwa Blog hii linasema
Watu wengi waliookoka hawajiingizi kwenye siasa hata kama wana wito huo kwa sababu
1. Uwoga wa kujaribu
2. Muda wake haujafika
3. Tulikuzwa kwenye mazingira ya kuwa siasa ni Dhambi
Unaweza shiriki kwa kupiga kura Hapo juu.
Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment