Kulingana na kuendelea kwa matumizi ya teknohama hapa nchini, kanisa la Tanzania nalo ni miongoni mwa sehemu ya maendeleo hayo. Hivyo ili kuwafikia watu wengi zaidi inalibidi kanisa nalo kukimbizana na kupanuka kwa teknolojia. Hii ni madhubuti kwa minajili ya kuokoa roho za watu pamoja na kuuimarisha mwili wa kristo. Kulingana na hitaji hilo, matumizi ya Tovuti hurahisisha kueneza injili kwa njia ya mtandao.
Wakati kanisani mhubiri anaweza hubiri na washirika wakaelewa ila wanaweza wakasahau kutokana na mrundikano wa mambo, hivyo endapo makanisa yatakuwa na utaratibu wa kupost mafundisho ya ibadani kwenye tovuti za kanisa hilo kutapanua wigo wa kujikumbusha kile kilichofundishwa ibadani na kuwasaidia wale ambao kwa namna moja au nyingine hawakuweza kuhudhuria ibadani.Hapa kwetu Tanzania kasi ya kutumia Tovuti na mitandao jamii kama mkondo mwingine wa kupeleka injili ni ndogo, wapo watumishi wenye kuamini tofauti na Tovuti(websites), kujiingiza kweye mitandao jamii ni dhambi na kama si dhambi basi mtumishi unakuwa unapoteza ushuhuda mtazamo ambao si sahihi ukilinganisha na kasi ya kukua kwa teknolojia duniani kote.
Japokuwa kasi ya kanisa la Tanzania katika matumizi ya Tovuti ni ndogo, ni jambo la kutia moyo kuona kuna makanisa ambayo yameliona hilo na yamejikita pia kuhakikisha yanaifikia jamii kubwa kwa neno la Mungu kupitia Website/Tovuti za makanisa hayo.
Changamoto kubwa iliyopo kwa makanisa yenye Tovuti ni kuwa nyingi haziboreshwi au kuwekewa vitu vipya(updated). Katika tovuti nyingi zilizopo utakuta vitu vilivyowekwa kwenye tovuti januari mpaka disemba vinakuwa kama vilivyo. Kwa utafiti wangu mdogo kwenye makanisa kadhaa yenye tovuti nimegundua sio kwamba wataalamu wa kuboresha tovuti hizo hawapo, laaa!!! Wapo, ila ni uzembe pamoja na kutotilia maanani uwepo wa website kama mfereji mwingine wa kuhudumia Roho za watu. Wengine Tovuti zipo kama sifa kuwa kanisa letu/langu lina tovuti hivyo linaenda na wakati ilihali tovuti ILIYOPO haikidhi haja ya kuzifikia ipasavyo Roho za watu.
Hosanna Inc imeandaa orodha ya Tovuti/Blog(website) za kikristo ambazo zipo hapa Tanzania na zingine za watanzania walioko nje ya nchi ambazo zinatangaza habari njema za Kristo Yesu.
Orodha hii itakuwa ikiboreshwa mara kwa mara ili kwenda na wakati, na kama ipo website au blog ya kikristo iliyoko Tanzania au ya watanzania/mtanzania aliyeko popote duniani yenye lengo la kumtangaza Kristo ambayo haijawekwa katika orodha hii, tafadhali wasiliana nasi ili tuijumuishe. Nia hasa ni kuwawezesha watanzania kuweza kujifunza Neno la Mungu kupitia tovuti hizo na kupata habari mbalimbali zinaouhusu mwili wa Kristo hapa nchini na Duniani kote.
Kazi yenu ni njema na awabariki;maana mmetusaidia kuliko mnavyoweza kufikiri.
ReplyDelete