Mathayo
17:12 “lakini namna hii haitoki, ila kwa kusali na kufunga”.
Mpenzi
msomaji naamini kwa sehemu huenda unaijua vizuri habari ya Mathayo 17:14-21
“Habari hii inahusu kijana mmoja aliyekuwa na pepo wa kifafa, wanafunzi wa Yesu
wakamwombea wasiweze kumponya. Yesu alipokuja toka mlimani akamponya yule
kijana. Baadae walipokuwa faragha wanafunzi walitaka kujua kwa nini wao
walishindwa kumtoa pepo. Yesu aliwapa sababu 2, moja kwa sababu ya upungufu wa
imani yao, na pili akawaambia namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.
Sasa
mwezi huu nataka tutafakari swali hili kwa pamoja, Je, ni wakati gani/au kwa
mahitaji gani unatakiwa kusali na kufunga? Hapa Yesu alimaanisha kuna
mambo/maombi mengine hayawezi kujibiwa mpaka kwa maombi ya kufunga.. Sasa swali
ni wangejuaje kwamba hitaji hili/namna hii inataka kusali na kufunga au
kusali bila kufunga.
Nina
amini hata msomaji wnagu una mahitaji mengi unayoombea, yapo ya kwako binafsi,
familia, kanisa, nchi, kazi, mume, mke, mchumba, biashara, watoto nk.
Hii
ina maana kuna baadhi ya maombi yako hayatajibiwa haraka au kabisa hadi uombe
na kufunga. Swali ni Je, unajuaje kwamba sasa natakiwa kusali na kufunga au
kusali bila kufunga.
Mambo
matatu yafuatayo yatakusaidia;
a)
Kutokuona matokeo ya maombi ya bila kufunga.
Hii
ina maana huenda kwa muda mrefu umekuwa ukiombea jambo fulani bila kuona
matokeo yake. Usibakie kusema kwamba natakiwa kuwa mvumilivu. Huenda hiyo ni
taarifa kwamba ndugu namna hiyo haitoki ila kwa kusali na kufunga. Hivyo ongeza
kufunga kwenye maombi yako, utaona matokeo yake kwa kipindi kifupi.
b)
Uzito na uharaka wa suala unaloombea.
Uzito
wa jambo unaloombea ni kwa mtu binafsi (too personal). Jambo ambalo kwako ni
zito/mzigo kwa mwingine si zito. Mfano suala la binti anayetafuta mume/mtu
anayetafuta kazi uzito wa hili suala hauwezi kulingana kati ya mtu na mtu.
Huenda huyu dada ameomba miaka 3 na hajaona mtu akija kumsemesha, kwa mtu huyu
tatizo hili ni zito sana. Hatua kama hii inamtaka afunge na kuomba.
Mfano
mwingine ni hatari ya kifo kama mazingira yaliyowakuta kina Esta katika utawala
wa mfalme Ahusuero, pindi ulipoandaliwa mpango wa kuua wayahudi wote, tunaona
walifunga kwa siku tatu, au watu wa mji Ninawi walipoambia na Yona kwamba
wasipotubu mji wao pamoja na wao wataangamizwa, nao walifunga. jifunze kwa
Esta, Daniel, Yona, Nehemia, Yesu n.k
c) Kwa
uongozi wa Roho mtakatifu.
Mathayo
4:1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani… akafunga siku arobaini …………”
Awali
ya yote kumbuka Roho mtakatifu ni msaidizi hata kuomba anatusaidia. Roho
mtakatifu ndiye anayeleta au kuweka mzigo wa kuomba ndani ya mtu. Roho
mtakatifu ndiye anayejua habari ya mambo yajayo, kwa sababu hiyo huwa
anamsukuma mtu kufanya maombi ya kawaida au ya kufunga tegemeana na hitaji
husika na kile kilichopo mbele ya mtu husika. Kwa lugha nyepesi Roho mtakatifu
humuongoza mtu katika maombi ya kawaida au ya kufunga pia.
Hivyo
basi Roho mtakatifu akikuongoza kufunga wewe usimzimshe au usikwepe maana yeye
anajua nini kinaenda kutokea mbele yako na kinahitaji nguvu kiasi gain ya
maombi ili uweze kuvuka au ili namna hiyo iweze kutoka.
Ni
imani yangu kuwa ujumbe huu mfupi utakusaidia kukujengea nidhamu katka maombi
yako kwa ujumla na utakuwa makini na maombi unayoyafanya.
Barikiwa
na Yesu kristo.
Mwl Patrick Sanga
Kuna Imani na kuamini(Faith and belief). Imani si tatizo kwa Wakristo na uhitaji Imani kubwa(Yesu anasema imani ndogo kama punje ya haradali yatosha).kUTOKUAMINI NDIO TATIZO,ndio maana Baba wa mtoto alijibu vile....help my unbelief.Na aliposema haiji ila kwa...ambayo haiji ni kuondoa kutokuamini sio kuondoa mapepo kwani kutokuamini ndio chanzo cha maombi kutojibiwa..Ubarikiwe mtu wa Mungu
ReplyDeleteHello Everybody,
ReplyDeleteBelow is a list of the highest ranking FOREX brokers:
1. Most Recommended Forex Broker
2. eToro
Here is a list of money making forex tools:
1. ForexTrendy - Recommended Odds Software.
2. EA Builder - Custom Indicators Autotrading.
3. Fast FX Profit - Secret Forex Strategy.
Hopefully these lists are helpful to you.