Friday, October 14, 2011

Harris Kapiga aelezea Changamoto Katika Kuuvusha Mipaka Muziki wa Injili


Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Tunzo za Muziki wa Injili, Haris Kapiga (Kushoto) akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA kuhusu Changamoto katika kuuvusha mipaka muziki wa Injili. Kulia ni Kaimu Mratibu wa Jukwaa hilo Aristide Kwizela.
Mmoja wa wanakamati wa Tuzo za Muziki wa Injili nchini NA MTANGAZAJI WA Clouds Fm Mtumishi Harris Kapiga alisema kuwa, kuna kila sababu ya wasanii wa muziki wa injili nchini kufanya kazi zao kitaalam zaidi na kutumia teknolojia ya mawasiliano katika kujitangaza. Kapiga alisema hayo kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki katika makao makuu ya Balaza la sanaa Tanzania{BASATA}.

Mtumishi Kapiga aliendelea kusema “Ni ajabu sana, kuna wasanii wengi wa muziki wa injili ni maarufu sana lakini hawapatikani kwenye mitandao kama ya Facebook, twitter na mingineyo ambayo hutumiwa na wasanii wengi katika kujitangaza” Kapiga.
Aliongeza kuwa, hali hiyo ni tofauti na wasanii wa nje kama Rebecca Malope ambao ukiingia kwenye mitandao ya mawasiliano ni rahisi sana kupata taarifa na hata kazi zao hivyo kutanua fursa zao za kujitangaza na kujipatia kipato.

Kuhusu utafiti alioufanya kwa kuzungukia maduka mbalimbali ya usambazaji kazi za Wasanii wa muziki wa Injili Bw. Kapiga alisema kuwa, wasanii kutoka nje kama wale wa Kundi la Ambassadors of Christ kutoka Rwanda na Sara K wa Kenya wamekuwa wakifanya vizuri na kuwazidi wasanii wa ndani.
Alitoa wito kwa wasanii kutumia fursa mbalimbali kujitangaza hasa kutumia teknolojia za kisasa na kutengeza kazi zenye ubora ili kazi zao ziweze kuvuka mipaka na kufanya vizuri zaidi.

Kwa uchunguzi uliofanywa na Hosanna Inc katika mitandao Jamii unaonyesha wazi kuwa wanamuziki wa injili hawajitangazi kupitia Mitandao Hiyo. Mpaka sasa wanamuziki wa Injili wenye  Kurasa au Account kwenye Facebook  na ambazo ziko Active ni pamoja na Upendo Kilahiro, John Lisu, J. Sisters, Jane Miso, Emmanuel Mabisa, Addo November, na Ambwene Mwasongwe na wengine wachache ambao hatujapata taarifa zao.Kwa Upande wa mtandao jamii wa Twitter Addo November ndiye Mwanamuziki wa Injili pekee kutoka Tanzania mwenye Account  katika mtandao huo.

Upendo Kilahiro na Addo November ndio wanamuziki wa Injili wanaoongoza kwa kuwasiliana na wapenzi wa Muziki huo kupitia account zao za Facebook.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...