Thursday, October 27, 2011

Wanamuziki wa Injili nchini Tanzania wakamilisha Video ya Wimbo wa Miaka 50 ya Uhuru.

Baadhi ya washiriki wa wimbo huo Mwl John Shaban kushoto, Martha Mwaipaja,Debora Said, Emmanuel Mgaya(Masanja),Mzungu Four Jane Misso na wengine wakiwa Makini katika shughuli hiyo

Hatimaye waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania wakiongozwa na mwalimu wa muziki Mtumishi John Shabani, chini ya usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita) wamekamilisha video ya wimbo ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. 

Pamoja na waimbaji mbalimbali kushiriki katika wimbo huo pia yumo mheshimiwa Martha Mlata ambaye amechangia sana katika kufanikisha kurekodi wimbo huo. Baadhi yam abo aliyo yafanya ni pamoja na kufanikisha kupata sare na bendera kutoka serekalini pamoja na kutoa feha za kufanikisha kurekodi video. Pia studio ya Pro arts studio ya jijini Dar es salaam ilijitolea kurekodi sauti. 

Video Ikifanyika

Wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili na kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru, lilianzishwa na bwana Tc Timothy Chelula na kumshirikisha mwalimu John Shabani, ndipo walipo kihusisha chama cha muziki wa injili na vyombo mbalimbali vya habari. Muda si mrefu wimbo huo utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:

 
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.


Pamoja na hayo, Viongozi wa chama chamuziki Tanzania, wanatoa wito wa waimbaji kujiunga na chama hicho kwani kuna faida nyingi za kujiunga na chama. Fomu zinapatikana sasa. kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0754 818 767 au 0716 560094
.

Clip za Video Zikiendelea Kuchukuliwa

1 comment:

  1. Naomba nisiseme sana, hadi niisikie hiyo nyimbo... ila uzoefu unaonyesha bado hatujakuwa wazuri sana kwenye nyimbo za pamoja. Hii sio nyimbo ya kwanza kwa wapendwa kuimba kwa pamoja, kuna ile ya kuombea Amani, ambapo wakina David Robert waliiandaa na waimbaji wengine wengi... kwakweli ilikuwa mbaya sana hata video yake haikukaa sana kupigwa kwenye media.hebu ngoja niisikie hii afu nitarudi

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...