Juliani akiwa ameshika Tuzo mbili za Kisima Music Awards alizokabidhiwa wakati wa Sherehe za Tuzo Hizo kwa mwaka huu wa 2011 |
Juliani
ni Mwanamuziki mahiri wa Muziki wa Gospel HipHop nchini Kenya.katika Tuzo
Kongwe nchini Humo zijulikanazo kama Kisima Music Awards zilizomalizika hivi
karibuni. Julliani pamoja na kunyakuwa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Gospel Hip
Hop, pia amefanikiwa kunyakuwa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Mwaka nchini humo
nafasi iliyokuwa ikiwaniwa kwa karibu na mwanamuziki Kidumu pamoja na Jaguar
anayetamba na Hit Song iitwayo Kigeugeu.
Kitendo
cha Mwanamuziki wa Injili kunyakuwa Tuzo
ya Mwanamuziki Bora wa mwaka nchini humo na kuwaweka kando magwiji wengi,
kimepelekea mwanamuziki Huyo kupata Zawadi ya Shillingi Million Moja ya Kenya
ambapo zawadi hii inaaminika ni zawadi kubwa ya kwanza kutolewa katika Tuzo za
Muziki nchini humo.
Julliani
mwenye umri wa Miaka 25 anatamba nchini humo na nyimbo yake ya Gospel iitwayo
“Barua ya Ocampo” inayogusa Medani za siasa za sasa za nchi hiyo. Baada ya
kupokea hundi ya pesa hizo Julliani alisema atatumia sehemu ya pesa Hizo katika
kuendeleza Project iitwayo “Kama Si Sisi”
ambayo amekuwa akifanya nayo kazi. Project Hii lengo lake kubwa ni kuwafundisha
vijana namna ya kuondokana na majanga mbalimbali yanayoweza kuwakumba katika
umri wa ujana.
No comments:
Post a Comment