Wednesday, July 13, 2011

Tofauti ya Mwili wa Kristo na Huduma


 Katika waefeso 4:11-12 “Naye aliita (huduma) wengine kuwa Mitume Manabii wainjilisti wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya Mungu itendeke ”

Hapo utaona huduma ni kazi (it’s a physical work which can be viewed by our optical eyes), na kusudi la huduma hizi imewekwa wazi hapo juu katika mistari hiyo ni ili MWILI WA KRISTO UJENGWE. Hivyo huduma zipo maalumu kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo na si mwili wa Kristo upo kwa ajili ya kuijenga Huduma.

Kutokana na maandiko hayo utaona Mwili wa Kristo ndio unaanza kupewa kipaumbele kwa kuwa huduma zipo ili kuutumikia mwili huu na si huduma kutumikiwa na mwili wa kristo. 

Ni jukumu letu kama watumishi wa Mungu kuzidi kuiona huduma kuwa ni ya Mungu kupitia Kristo Yesu na si mali zetu binafsi, tusione tunaweza kujiamlia lolote juu ya huduma hizo kwa kuwa tu sisi ndio waanzilishi hivyo lolote tunalosema ni amri.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa ni kawaida kuona au kusikia mtumishi fulani akimponda mtumishi mwingine iwe kupitia madhabahu ya kanisani kwake au kwenye vyombo vya habari, ni vizuri tujiulize huduma hizi ambazo zimo ndani ya watumishi hawa ni za nani? na lengo lake hasa ni nini?, Kama lengo la pande zote hizi mbili ni kuujenga mwili wa Kristo sasa kwa nini tulumbane!!

au tunataka kuwaaminisha watanzania kuwa huduma yangu inanguvu au ni ya kiroho kuliko ya flani?, Kama wote lengo letu ni kuujenga mwili wa Kristo basi tusilumbane na tupige kazi kwa utukufu wa Mungu na sio kutimiza matakwa yetu binafsi, au tumesahau hekima iliyopo kwenye vile vitendawili vya kitoto kuwa “Pita huku nami nipite huku tukutane katikati !!!”

Ujenzi wa Mwili wa Kristo unanguvu mno kuliko ujenzi wa huduma, leo hii mambo ni tofauti kwa kuwa wapo watumishi wa Mungu wenye kuziweka huduma zao mbele kuliko Mwili wa Kristo, na kuna wengine wamefikia kuzifanya huduma hizo kama mali zao binafsi kitu ambacho sio sahihi. Nafurahi na kutiwa moyo kwa kuwa wapo ambao wanajua uthamani wa Mwili wa Kristo na wameupa kapaumbele kuliko huduma zao, na hao ndio kioo kwa wengine na mfano wa kuigwa.

Kama watumishi waMungu ni lazima tujue nini wajibu wetu kwa Mungu na pia tujue nini mipaka yetu kwa Mungu ili tuweze kufikia lengo la kuwepo kwa hizi ofisi (huduma). Ni kweli mtumishi anaweza fanya anavyotaka pasipo kuisikiliza sauti ya Mungu, lakini madhara yake yanaweza yasionekane leo wala kesho lakini kwa kuwa kuna siku alipanda hivyo kuvuna ni lazima endapo hakuomba rehema juu ya hilo.

Tunapofanya kazi yoyote ya Mungu maadamu Mungu katuweka katika eneo hilo iwe uimbaji, ushemasi, ualimu wa watoto kanisani, au kazi yoyote yenye lengo la kuujenga mwili wa Kristo ni lazima tukumbuke  hiyo kazi sio yetu ni ya Mungu, kwa kufanya hiyvo itatusaidika kunyenyekea mbele za Mungu na kujichunguza endapo tupo tukiendeleze kufanya tulichoitiwa au tayari tuko nje ya mstari hivyo turudi.

Mboya V.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...