Sunday, June 12, 2011

Baada ya miaka ya 21 ya Ahadi Askofu Mwakiborwa Apata Mtoto

Mch Bruno Mwakibolwa Kushoto akiwa mtaani na Mmoja wa washirika wake Bw Masanja Mkandamizaji wakihubiri Injili, Mchungaji Mwakibolwa hutimia gari lake binafsi pichani aina ya Fuso kuzunguka mitaani na kuhubiri

Askofu Bruno Mwakiborwa wa kanisa la Evangelical Assemblies Of  God Tanzania(EAGT), ambaye pia ni Mchungaji kiongozi wa kanisa la Mito ya Baraka lililoko maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam, amefanikiwa kupata Zawadi ya mtoto wa kike toka kwa Mungu waliyempa jina  la “Gwandumi” yaani Malaika.

Akitoa shukrani hizo mbele ya kanisa akiwa pamoja na mkewe, Mchungaji Mwakiborwa  mwenye umri wa miaka 59 alisema mnamo tarehe 26-12-1990 miezi miwili mara baada ya kuokoka Mungu alimwambia kuwa atampa mtoto wa kike , na jina lake atamwita Gwandumi kwa kiswahili Malaika ahadi ambayo haikuwa rahisi kuiamini kwa kuwa alikuwa mchanga kiroho lakini aliamini hivyo kwa kuwa Bwana ndio alisema.

Baada ya miaka mingi kupita, mwaka jana 2010 akiwa nchini Israel Katika jiji la Jerusalemu wakati wa kutoa sadaka, aliamua kumtolea Mungu SADAKA ya Dola za Kimarekani Mia Moja (100). Baada ya  sadaka hiyo kwa kuwa alikuwa na maombi ya uchungu juu ya hilo ndipo Bwana Yesu akamwambia “Nimesikia Maombi yako”.

Tarehe 31/05/2011 ikiwa ni miezi tisa toka atoe sadaka kwa Bwana ndipo mtoto akazaliwa katika Hospitali ya Regent iliyoko Upanga jijini Dar es salaam. Akasema kwa mtu aliyeokoa ni vizuri unapofanya maombi, hakikisha unapeleka na sadaka kwa Mungu.

3 comments:

  1. ameeen ukitaka kumjaribu Mungu toa dhaka sadaka na fungu la kumi

    ReplyDelete
  2. ameeeeeeeni askofu!...MUNGU ANAWEZA KUFANYA LOLOTE!!!!
    injili lazima ihubiliwe!!!

    ReplyDelete
  3. Alitoa USD 1000 na sio USD 100

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...