Basil Kashumba maarufu kama K`Basil ni mwanamuziki wa nymbo za injili ambapo hapo awali alikuwa akiimba nyimbo za kawaida(kidunia). K`Basil ambaye ni mhitimu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam(UD), nyimbo yake na Stara Thomas iitwayo Riziki ilimpatia ummarufu sana kisha akakaa kimya kwa muda wa takribani miaka mitano. Baadae mwaka 2008 akaamua Kumpa Yesu maisha yake(kuokoka). Kwa sasa yuko mbioni kutoa album yake ya kwanza ya muziki wa Injili.
Basil Kashumba |
Album yake ya muziki wa Injili iko tayari na sasa ameanza kufanya matamasha ya uzinduzi wa album yake hiyo ya kwanza ya muziki wa Injili aliyoipa Jina la Yesu Ananipenda akizunguka mikoa karibuni yote aliyowahi kupita kutumbuiza wakati akiimba muziki wa Bongo Fleva.
Tamasha lake la kwanza la Uzinduzi litafanyika mkoani Iringa, siku ya Jumapili ya tarehe 5 Juni ya mwaka 2011 na baada ya hapo K’Bazil atazunguka mikoa mingine kama Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na mikoa mingine michache. Awali tamasha hilo lilipangwa kuanza kufanyika May 29 ila ratiba ilisogezwa mbele kwaajili ya maandalizi zaidi. Tamasha hilo ambalo linaandaliwa na kuratibishwa na Blog site ya Ufufuo Music & News litakuja kumalizika katika mkoa wa Dar es salaam kipindi cha mwezi wa July baada ya kupita mikoa karibuni yote.
Nae mkurugenzi mtendaji wa Blog site ya Ufufuo Music & News inayojishughulisha na kazi ya kuwatangaza waimbaji wa Muziki wa Injili kwa kuandika habari zao pamoja na kutoa sapoti nyingine tofauti tofauti, ndugu Crispin Challe amesema kwamba ni furaha ya pekee na neema ya Bwana Yesu kwa K’Bazil kuitwa kuwa mtumishi wake. Nae kama mpendwa na mwokovu pia anafurahia kumtia moyo na kumuunga mkono K’Bazil kwa hatua aliyoifikia ya kuamua kumtumikia Mungu kwa moyo na kweli, kama mlivyosikia ya kwamba mbali na uimbaji K’Bazil pia ni mchungaji, alisema Crispin.
Kutoka kushoto ni Christina Shusho, Upendo Nkone na Stara Thomas,Stara Thomas nae inasemekana miezi kadhaa iliyopita aliyasalimisha maisha yake kwa Yesu. |
Album ya Injili ya K’Bazil inakwenda kwa jina la “Yesu Ananipenda” yenye nyimbo takribani 10 ambazo majina yake ni Namjua, Wakati Na Bahati, Wewe Ni Baba, Rudisha, Utukuzwe, Moyo, Asante Yesu, Tusonge Mbele, Mama na Yesu Ananipenda ndio nyimbo iliyobeba jina la album.
No comments:
Post a Comment