Mwl Silvester Gamanywa |
Aidha ni lazima tujue kwamba imani sio kitu cha kumshinikiza Mungu kuwa ni lazima!, lazima!, lazima!!! Hata kama tutanukuu vifungu vya maandiko na kuvifanya kama kigezo cha kumshinikiza Mungu ili afanye vile tunavyoomba.Ukweli unabaki pale pale kwamba Mungu hatekelezi amri ya kiumbe wake.
Nasisitiza katika hili maana siku hizi jamii yetu imejaa waumini wengi wenye utovu wa Nidhamu wa hali ya juu kiasi cha kumwamrisha Mungu ajibu maombi yao , tena kwa jinsi wanavyotaka wao. Na pengine wengine wao huenda Mungu aliwahi kuwajibu Maombi yao pindi walipokuwa bado wachanga kiimani(Kiroho). Lakini wao wakadhani ndio mtindo wenyewe kumfokea na Kumgombeza Mungu ili ajibu Maombi yao .
Ndugu zangu pamoja na kwamba Mungu huchukuliana na udhaifu wetu, lazima tujue hii huwa ni kwa Muda kitambo, na anao ukomo wa kuchukuliana na ujinga na uchanga wetu.
Mwl Silvester Gamanywa
No comments:
Post a Comment