“Twakupa sifa eeh Bwanaa, Milele, Milele, Milele, shaangwe, shaangwe Milele Milele Milele” hii ni nyimbo iliyogusa wengi usiku huo na kupelekea sifa kubwa kwa Mungu wetu. Lilikuwa tamasha maalumu la kufunga mwaka wa masomo wa 2010/2011 kwa wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustino maarufu kwa jina la Saut. Tamasha hili la kusifu na Kuabudu liliandaliwa na Tafes na lilihusisha vikundi mbalimbali vya kusifu na kuabudu vilivyo ndani na nje ya chuo hicho.
Pamoja na Kusifu na kuabudu pia KWAYA ya Tafes Saut usiku huo iliweka wakfu album yao ya pili ya muziki wa injili. Kwaya hiyo iliyo chini ya Mwl Mugisha Rweyemamu ambaye pia ni Lecturer wa chuo hicho ilionekana wazi kuwa ilikuwa imejipanga vyema kwa ajili ya shughuli hiyo. Maombi Rasmi ya kuiweka wakfu album hiyo yalifanywa namlezi wa Tafes Saut Dr Elikioni.
Praise Team ya Saut pamoja na Kundi maarufu la kusifu na kuabudu jijini Mwanza liitwalo Kingdom Worshipers ndio walioendesha zoezi zima la kusifu na kuabudu kwa usiku wote kuanzia saa Mbili usiku mpaka saa Tisa usiku ambapo zoezi hilo lilifungwa rasmi.Tamasha hili lilifanyika nje na sio ndani kama ilivyozoeleka na wengi kwa kuwa hakuna ukumbi chuoni hapo wa kuwaacomodate watu wengi kiasi hicho.
|
Mwenyekiti wa Tafes Saut Pastor David Mwakyusa akifanya maombi kabla ya tamasha kuanza |
|
Easther ni mmoja wa Praise team toka tafes saut, hapa akilead praise,kama ulishuhudia Tamasha la Tuzo za Muziki wa injili Tanzania 2011, dada yake aitwaye Mercy alimba wimbo wa N`gangania |
|
Emmanuel Landei toka Marafiki Gospel Group akiwa on Stage | | |
|
|
Aaah Kazi yako njema sana
ReplyDeleteMungu ni Mwema
ReplyDelete