Bwn Harold Camping |
Historia ya Halord Camping
Halord camping alizaliwa tarehe 19/07/1921 katika jimbo la kolorado nchini Marekani, akiwa angali mdogo yeye pamoja na wazazi wake walihamia katika jiji la Califonia. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari alipofika katika jiji la Califonia alipata fulsa ya kujiunga katika chuo kikuu cha Califonia ambako alisomea masomo ya uhandisi wa Majengo(B.S in Civil Engeneering) na kumaliza mwaka 1940. Mnamo mwaka 1943 alifunga ndoa na Shirley Camping ambaye ndiye mkewe mpaka hivi leo.
Maisha ya Kiimani
Camping kwa muda mrefu alikuwa muumini wa kawaida wa kanisa la Christian Reformed Church hadi mwaka 1988 alipopewa cheo cha uzee wakanisa na Mwalimu wa shule ya jumapili .
Umilikaji wa vyombo vya habari
Mnamo mwaka 1958 Bw Camping aliungana na wenzake waliokuwa wakiabudu katika makanisa ya Christian Reformed, Bible Babtist, na Conservative Christian Presbyterian na kununua kituo cha Redio katika jimbo la San Fransisco jijini Califonia ,Redio hiyo ya FM ilijulikana sana kwa jina la KEAR Family Radio. Lengo lao hasa lilikuwa ni kutangaza injili ya Yesu Kristo. Kituo hicho cha redio kilifanikiwa kukua kwa kasi, hadi kufikia miaka ya 1960 Family Rdio ilizaa Redio nyingine za FM zipatazo sita, na vituo vingine saba vilivyokuwa vikirusha matangazo katika masafa ya AM pamoja na usambazaji wa ijili kupitia Mtandao.
Camping alianzisha kipindi cha maswali na majibu kupitia redio hiyo,ambapo wasikilizaji walikuwa wakiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maana ya vifungu mbalimbali vya kwenye biblia,matatizo ya kifamilia na kijamii na Camping alikuwa akiwapa majibu kwa mujibu wa Biblia. Kipindi hiki kilimuongezea sana umaarufu.
Wafuasi wa Camping wakiwa Mitaani wakieneza habari za unyakuo wa tarehe 21 May 2011 |
Harakati za kutoa Unabii
Camping baada ya kupata umaarufu wa kutosha, alianza kutoa tabiri mbali mbali zenye kufuata hesabu za kibiblia.Tabiri hizi alikuwa akizitangaza kwa nguvu sana kupitia vyombo vya habari na hivyo kumzidishia umaarufu. Tarehe 21 May mwaka 1988 alitoa unabii kuwa Kristo atalinyakua kanisa unabii huu haukutimia. Kama vile haitoshi Mwaka 1994 kwa mara nyingine tena Bw Camping alitoa unabii kuwa Bwana Yesu atakuja kwa ajili ya kulinyakuwa kanisa. Katika unabii huo alidai tukio hilo la Yesu kuja litatokea mnamo mwezi wa tisa mwaka huo wa 1994.Unabii huo pia haukuweza kutimia.
Baada ya kimya cha miaka takribani sita ndipo mwaka jana mwishoni akaja na utabiri mpya kuwa mwaka huu tarehe 21 may 2011, Kristo atakuja kulichukua kanisa lake yaani watakatifu. Unabii huo ulizidi kufafanua kuwa baada ya watakatifu kunyakuliwa ,na dunia kubaki na wenye dhambi, itapofika tarehe 21 /10/2011 Dunia itafikia ukingoni na kutakua hakuna maisha tena chini ya jua.
Katika awamu hii ya unabii Halord Camping alitumia nguvu nyingi katika kuutangaza unabii wake na alifanikiwa kufikisha ujumbe katika sehemu kubwa ya Dunia ukilinganisha na nabii zilizopita. Pamoja na utabili huo pia Camping alitanabaisha kuwa watu takribani Millioni mia mbili (200) sawa na asilimia tatu(3%) ya watu wote duniani ndio watanyakuliwa.
Mmoja wa wafuasi wake |
Uchangiaji Pesa kwa ajili ya kusambaza Habari
Family Radio imetumia zaidi ya Dola za kimarekani million mia moja kwa ajili ya kusambaza ujumbe wa kuitahadharisha dunia, na camping aliweka nguvu katika hili kwa kuwa aliamini Yeye anachofanya ni kama Nuhu ili watu waelewe lazima wasikie habari hizo kwa gharama yeyote. Maelfu ya watu walichangia mali zao na pesa zao ili kufanikisha hilo zoezi. Bwana Robert Fitzpatrick ambaye ni mstaafu na mfuasi wa Camping alitumia Dola za kimalekani 140,000/=pesa yake aliokuwa akiitunza kwa muda mrefu kwa ajili tu ya kumsapot Bwn Camping.
Bwana Matt Tuter ambaye ni Program Manager wa Family Radio alisema, pamoja na kwamba watu walichangia juu ya jambo hilo ila kiasi kikubwa cha pesa kilipatikana mara baada ya Family Radio kuamua kuiuza Television yao iliyojulikana kama KFTL TV pamoja na kituo kimoja cha Radio chenye kurusha matangazo yake kwenye masafa ya FM.
Tuter aliendelea kusema pamoja na kufanya kazi chini ya Bwn Camping, wengi wa wafanyakazi wa Family Radio hawakubaliani na kampeni za bosi wao,na hii ni pamoja na yeye mwenyewe Tuter.
Campeni za Halord Camping nchini Tanzania
Bwa Camping pamoja na kufanikiwa kusambaza taarifa karibu sehemu kubwa ya Dunia, nchini Tanzania alituma wawakilishi wake ambao walitembea hususani kwenye miji mikubwa nchini na kusambaza habari za unyakuo huo. Jijini Dar es salaam walifanikiwa kuweka mabango makubwa mawili wilaya ya Kinondoni, pamoja na wilaya ya Ilala eneo la Feri. Kwenye mikoa ya Arusha na Mwanza wawakilishi hao kwa kushirikiana na watanzania wachache, waligawa vipeperushi, na hili lilifanyika siku chache kabla ya tarehe 21 May 2011.
Harold Camping akiendesha kipindi chake cha Television |
Kauli ya Bwn Camping baada ya Unyakuo Kushindikana
Jumatatu ya tarehe 23/06/2011 akiwa amevaa tishirt na jacket siku mbili baada ya tukio la unyakuo kushindikana, Bwn camping mwenye umri wa miaka 89 alitoka nje ya nyumba yake na kukutana na umati wa watu pamoja na waandishi wa habari.Alianza kwa kusema weekend hii imekuwa ngumu sana kwangu, akasema na haya yote Family Radio haikuyafanya ili kupata malipo ya aina yoyote, na Family Radio iko makini na inafanya kazi kwa uwazi sana hususani kwenye eneo la fedha.
Camping akaendelea kusema, michango yote ambayo waliipokea waliielekeza kwenye eneo husika.Aidha Bwn Camping alipoulizwa nini hatima ya wafuasi wake ambao wengine waliamua kuacha kazi zao na kumuunga mkono katika kusambaza habari za unyakuo ila kwa sasa maisha yao kifedha si mazuri, Camping alijibu kuwa Taasisi yake haikuwahi kumshawishi mtu yeyote aache kazi bali waliacha kwa matakwa yao na alikataa kubeba jukumu lolote juu ya hali ya kifedha waliyonayo wafuasi wake kwa sasa.
No comments:
Post a Comment