Pastor Eliud Mwasenga |
Luka 8: 40-50
Katika mistari hoyo tunamuona Yairo, aliyekuwa na binti yake mgonjwa na kuamua kutafuta msaada toka kwa Yesu.Wakati anamwambia Yesu Matatizo yake kwa namna ambavyo Yesu alikuwa akimjibu alifikiri labda Yesu hatilii maanani tatizo lake.Na wakati huo huo Yairo akaletewa habari kutoka nyumbani kuwa Binti yake amefariki. Alipomwambia Yesu mtoto amefariki Yesu akamwambia MTOTO HAJAFARIKI.
Unaweza kuona namna ambavyo mazingira yanasema wazi kuwa mtoto amefariki lakini Yesu anapingana na Mazingira hayo. Hata siku moja usiyatii Mazingira ila amini katika kile Yesu asemacho juu ya Mazingira hayo. Kwanza unatakiwa kuchagua kuamini katika Neno la Mungu inawezekana ni kweli kabisa umefeli mitihani darasani, au biashara haiendi vizuri, au mwili haujisikii vizuri kisha kumbuka kile ambacho Mungu amesema juu ya eneo hilo na ndicho ukitamke.
Ebrania 12: 1 Kwa kuwa tumezungukwa na mashahidi wengi, katika yale tunayoyafanya japokuwa ni changamoto kwetu lazima tujue kuwa tumezungukwa na mashahidi wengi ambao wanakutarajia wewe ushinde ili nawao waweze kupenya kwenye maeneo yao, Hivyo ni Lazima ushinde. Haijalishi unapitia wapi na nini, chagua kutomungusha Mungu kwa kuwa anategemea wewe ushinde.
Yezeberi alimtisha Eliya kwa kumwambia kuwa atamuua, na Eliya hofu ilimjaa akatishika na akaamua kwenda kujificha mapangoni ili asikutane na mkono wa Yezeberi. Alipokuwa yuko pangoni Mungu alimwambia toka huko.Na hivi leo Mungu bado anasema toka kwenye hali uliyonayo kwa kuwa mimi nipo kukupa msaada.
Wakati Goliath aliposimama na kuanza kulitukana Jeshi la Mungu, Daud hakukaa kimya, japokuwa Goliath alikua tishio kwa wayahudi wote, lakini pindi alipoanza kutukana Daudi alikumbuka Matendo makuu ya Mungu na hivyo hakukaa kimya akasema wewe ni nani hadi utukane majeshi ya Mungu aliye hai.Hivyo wakati uko vitani sema na kumbuka ukuu wa Mungu kwa kuwa katika hiyo vita uliyopo Mungu anatarajia Lazima Uishinde kwa kuwa yeye yuko upande wako.
By: Pastor Eliud Mwasenga
No comments:
Post a Comment