Sunday, September 9, 2012

Kutoka Magazeti ya Kikristo Jumapili hii kwa Ufupi


 
Gazeti la


Onyo: Kimbunga cha Katrina na Isaac ni Matokeo ya Uasi
Maangamizi makubwa yanayotokana na Vimbunga viwili vya Katrina na Isaac vilivyotofautiana miaka saba  imeeelezwa kuwa ni uharibifu uliotokana na hasira ya Mungu baada ya wanadamu kufanya matamasha makubwa ya Ushoga na uasi wa maadili uliopindukia.Watu hao walifanya sherehe kabambe ambayo ilijumuisha jumla ya watu 120,000 katika mji wa New Orleans sherehe hizo hufanyika baada ya miaka saba na ilibuniwa tangu mwaka 1972 na kukua taratibu.

Kikongwe mmoja mkazi wa eneo la New Orleans alisema hayo kufuatia kimbunga kutokea na kuwapiga, mji huo umekuwa mwenyeji wa sherehe hizo. kikongwe huyo aliongeza kuwa mi naona Mwisho unakaribia na uvumilivu wa Mungu juu ya Taifa la Marekani unafikia mwisho.


Jumapili ya Kihistoria ndani ya  Victory Christian Centre Tarbenacle(VCCT)
Kwa mara ya Kwanza kanisa la Victory Christian Centre Tarbenacle(VCCT) lililofahamika zamani kama Victory Christian Centre (VCC) limefanya ibada yao ya kwanza katika hema lao kubwa baada ya kuhamia rasmi.Kanisa hilo kwa sasa limehamia maeneo ya Mbezi Beach “A” na zamani lilikuwa katika ukumbi uliopo kituo cha Petroli cha Victoria jijini Dar es salaam.


Hema la Jipya la VCCT
Katika Ibada hiyo ya kipekee kila mtu aliinua sauti yake na kumtukuza mungu kwa ukuu na wema wake huku mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Dr Huruma Nkone alisema kuwa hayo ni matokeo ya baraka nyingi ambazo Mungu amewajalia kwa kununua kiwanja na kusimika hema la kuabudia lenye uwezo wa kubeba jumla ya watu zaidi ya 1000. Akitoa historia fupi ya kanisa hilo Dr Nkone alisema kanisa hilo lilianza mwaka 2005 na jumla ya watu 15 katika maeneo ya Muhimbili eneo la Scripture Union kisha likahamia katika ukumbi wa  kituo cha Petroli cha  Victoria na kwa sasa kanisa hilo lina zaidi ya washirika 1000.

Kanisa Lazindua siku 90 za Usomaji wa Biblia
Kanisa la TAG Changanyikeni Kizota jijini Dar es salaam limezindua siku 90 za kuchunguza maandiko ya Biblia ili waumini wake waweze kuwa imara katika kuisimamia Imani ya kweli ya Kristo Yesu, kama walivyofanya wana wa Beloya waliokuwa shupavu katika kuchambua maandiko.Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Mchungaji wa kanisa hilo Mch Emmanuel Sote alisema waumini wamekuwa wakisoma Biblia zao kama kawaida lakini la kusoma katika muda wa siku 90 zitaleta ari mpya ndani yao.

Mchungaji huyo amesema kuwa ingawa zoezi hilo litakuwa la miezi mitatu lakini kutafanyika zoezi la kufaya tathmini kuweza kujua wapi mtu hajaelewa au wapi panahitaji ufafanuzi ili mwisho wa zoezi hilo kila mtu aweze kutoka na kitu cha Ziada.

Ndondodoo Kutoka Jibu la Maisha
Zitto alia na uchache wa wataalamu wa gesi
Casfeta kuleta ukombozi kwa vijana
Ni nani ambao hawataonja umauti mpaka wauone kwanza ufalme wa Mungu?..(2)
Mungu anashughulika na Mavazi tunayovaa?


Gazeti la
Nyakati 
Gazeti huru la Kikristo la Kila wiki


Wanasayansi wadai Jua Kuzimika Dunia Nzima Dec 2012
Watafiti mahiri duniani wa mambo ya anga kutoka nchini Marekani(NASA) wanadaiwa kuchunguza na kubaini kuwa mnamo Desember 23-25 mwaka huu wa 2012 jua litazimika kama ilivyokuwa wakati Yesu anasulubiwa msalabani.Kama taarifa hiyo kutoka kwa NASA itakuwa ya kweli mabilioni ya watu watalazimika kusherehekea sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu(Christmass) wakiwa wangali gizani.

Kwa mijibu wa NASA Ndani ya siku hizo jua litashindwa kutoa Nuru yake na hivyo kutakuwa na giza totoro.Kwa mujibu wa wasanyansi hao ni kuwa dunia itahama kutoka hapo ilipo sasa ambapo kwa kipimo cha kisayansi kinaitwa “Three Dimension” na kwenda katika kipimo cha “Zero Dimension”.Wanasayansi hao wanadai katika kipindi hicho dunia nzima itakabiliwa na mabadiliko makubwa na hatimaye kutashuhudiwa dunia mpya kabisa ikiumbwa.

Bahati Bukuku Hajafa
Watu wasiofahamika na ambao malengo yao hayajafahamika juzi jumanne iliyopita(04/09/2012)  walieneza uvumi kuwa muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Bahati Bukuku kuwa amefariki dunia kwa ajali barabarani.Uvumi huo ulisambaasana kwa njia ya ujumbe mfupi na kituo kimoja cha redio nchini kilipiga simu katika chumba cha habari cha gazeti la Nyakati ili kujua kama habari hizo ni za Ukweli.

Bahati Bukuku
Baada ya taarifa hizo gazeti la Nyakati lilifanya utafiti na hatimaye lilipata nafasi ya kuongea na Bahati Bukuku mwenyewe na kuthibitisha kuwa yuko hai na muda huo alikuwa maeneo ya Mabibo studio akirekodi video ya album yake ya mpya iitwayo Dunia Haina Huruma.

Askofu ahoji Wazinzi kutengwa wasiotoa zaka kuachwa
Askofu wa kanisa la International Evangelism Sinai askofu Silvester Thadei amewataka watumishi wa Mungu kuacha kabisa kukemea na kuchagua dhambi za kukemea na kutenga waumini pindi wanapokiuka misingi ya Kiroho.Askofu Thadei huchunga kanisa la “Mlima wa Bwana”  lililoko Ipagala mjini Dodoma, askofu huyo  aliyasema hayo wakati akihubiri kanisani hapo jumapili iliyopita.

Akitoa mfano askofu huyo alihoji  mantiki ya baadhi ya viongozi wa dini kukemea na kuwatenga waumini waliofanya dhambi ya Uzinzi huku wakiwaacha bila kuwakemea waumini wasiomtolea Mungu fungu la Kumi. Ikiwa wote hao( wazinzi na wasiomtolea Mungu fungu la kumi) wote wamemkosea Mungu kuna sababu gani ya watumishi wa Mungu kukemea dhambi moja na nyingine kuachwa bila kuchukuliwa hatua stahili alihoji askofu Dhadei.

Jenipher Mgendi kutoa Filamu Kuiponya Jamii
Muimbaji wa nyimbo za Injili na muaandaaji wa filamu za kikristo nchini mtumishi Jenipher Mgendi amekamilisha Filamu nyingine iitwayo CHAI MOTO.Hii ni filamu ya nne kutoka kwa mwanamama huyo  ikitanguliwa na Joto la Roho,Teke la Mama, pamoja na Pigo la Faraja.Mgendi ameliambia gazeti la Nyakati kuwa filamu hiyo ni ya dakika 115 na kwa sasa tayari ipo madukani.

Jenipher Mgendi
 Kwa mujibu wa Mgendi filamu hiyo inazungumzia changamoto mbalimbali zilizopo katika maisha ya ndoa na hasa pale wanandoa wasipompatia Mungu nafasi ipasayo.Filamu hiyo imeongozwa na Christian Mhegga na Mgeni Hamisi huku wahusika wakiwa ni Jenipher Mgendi mwenyewe, Musa Banzi, Juma Mtima, Christine Matai,Yvyone Cheryl maarufu kama monalisa na wasanii wengine wengi.

Ndondoo kutoka Gazeti la Nyakati
Nabii apinga kuombea Adui
Wasio na mafanikio hawalijui Neno
FPCT Sombetini Arusha kupanua eneo lao
Jaji Warioba - Waacheni wanachi wachangie Maoni yao juu ya katiba

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...