Wednesday, July 11, 2012

Anayetuhumiwa Kuvamia Kanisa La KKKT Iringa Afikishwa Mahakamani
Pichani ni Lawarance Mtatifikolo (30) Mkazi wa Image wilayani Kilolo, mkoani Iringa ambapo jana mtuhumiwa huyo Mtatifikolo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mjini Iringa akituhumiwa kufanya fujo kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu namba 170 cha Kanuni ya Adhabu.

Katika mahakama hiyo ilielezwa kwamba mnamo Julai 8, mwaka huu , Mtatifiko akiwa na wenzake wanne (hawajakamatwa) walifanya kitendo kisichoruhusishwa kisheria kwa kufunga mlango wa kanisa na kusababisha usumbufu kwa waumini.

Walifunga lango kuu la kuingilia Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Iringa wakilenga kufikisha ujumbe kwa Askofu wa Dayosisi hiyo kwamba hawataki aendelee kuwa kiongozi wao kwasababu anatuhuma nyingi za kimaadili na uongozi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Festo Lwila itatajwa tena mahakamani hapo Julai 24 wakati uchunguzi wake ukiendelea

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...