Thursday, July 5, 2012

Glorious Celebration waja na Ring-Tones za Album yao kwa watumiaji wa mtandao wa TigoThe Most leading upcomming gospel group in Tanzania known as Glorious Celebration sasa wamekuja na zawadi njema kwa watumiaji wa mtandao wa TIGO.Akiongea na Hosanna Inc mmoja wa Viongozi wa kundi hilo Mtumishi wa Mungu WISEMEN Emmanuel Mabisa amesema, kuanzia sasa kama unataka kuwa na Ring-tone za nyimbo za Glorious Celebration wakati wa kupokea na Kupiga simu unaweza andika Code zanyimbo hapo chini na kuzituma kwenye namba 15050

Niguse  -  18486
Unaweza – 18485
Eeh Roho – 18490
Eeh Nasfi – 18491

Hii ni fursa kubwa kwa wapenzi wa muziki wa injili nchini kupata nafasi ya kuwa Ma-DJ wa nyimbo wazipendazo kutoka kwenye kundi hilo kwa kuwa unaweza kubadilisha Ring-Tone kadri uwezavyo kwa kuandika tu Code ya nyimbo hapo juu na kisha kuituma kwenye namnba 15050  na utakatwa Shilingi 300/=. 

Glorious Celebration linakuwa ni kundi la Kwanza la Muziki wa injili nchini kuingiza nyimbo zao ZOTE kwenye mtandao wa Tigo na kuwawezesha watu kubarikiwa na nyimbo hizo kama Ring Tones.

Hapa nchini kwa upande wa Gospel Music tumeshuhudia Ring-Tone nyingi ni  za wanamuziki binafsi (Solo-Artists) na sio za Makundi kama Kwaya na bendi.Kingine katika hili ni kwamba hata wanamuziki binafsi wa injili wengi wamepata nafasi ya kuweka Ring-Tone ya nyimbo zao chache na nyingi ni zile zilizo HIT na sio zote(album nzima) kama walivyofanya Glorious Celebration.Kila Safari ndefu huanza na hatua kwa hili Glorious Celebration wamefungua njia. 

Kwa mujibu wa Mabisa amesema huu ni mwanzo tu na wanatarajia siku za hivi karibuni kupanua  wigo na kuwawezesha watumiaji wa mitandao mingine ya simu kupata huduma hii.Kwa sasa kundi hilo lime-reliase Codes za baadhi ya nyimbo na siku za hivi karibuni wataachia codes za nyimbo zilizobaki ingawa Hosanna Inc imepata bahati ya Kuziona Codes za Album yao yote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...