Wednesday, July 4, 2012

Historia ya mtumishi Kekeletso Phoofolo kutoka South Africa


Kekeletso Phoofolo
 
* Kekeletso maana yake Maongezeko

* Baada ya Tour yake na Dube ilimtoa kwa kiasi kikubwa kwa kumfanya ajulikane na kujiunga  na Joyous Celebration

* Uwezo wake wa kuimba, kulimiliki jukwaa, pamoja na Kuhubiri kwa Nguvu kubwa za Roho mtakatifu ndivyo vitu vinavyomtofautisha sana Keke na Mwanamuziki yeyote umjuaye wa nyimbo za Injili Duniani.

Kekeletso Phoofolo ama “KEKE” kama ajulikanavyo kwa wengi Barani afrika na Duniani kote ni Mwanamuziki  wa Muziki wa Injili kutoka nchini A frika ya Kusini. Kekeletso maana yake Maongezeko, Keke alizaliwa katika kitongoji cha Pimville kilichoko Mjini Soweto nchini Afrika ya Kusini. Kadri alivyokuwa akikuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kujiunga na Jeshi la nchi hiyo.Ndoto yake hiyo haikuweza kutimia kwa kuwa pamoja alikuwa akipenda jeshi pia alikuwa akipenda sana muziki.

Mwaka 1994 Keke alianza rasmi kujishughulisha na Muziki ambapo alijiunga na kundi la Zoe Gospel Music akiwa kama Back Vocalist. Mwaka 1997 Keke alikuwa na uwezo wa kufanya kazi zake binafsi akiwa kama Solo artist. Wakati akifanya kazi zake binafsi  mnamo mwaka 1998 alipata tena nafasi ya kujiunga na kundi lingine la Muziki wa injili nchini humo lijulikanalo kama Kom Kom. Mwaka 1999 Keke alipata nafasi ya kufanya Tour na Nguli wa Muziki wa injili nchini humo Benjamini Dube.

Keke on Stage
Baada ya Tour na Dube ambayo ilimtoa kwa kiasi kikubwa kwa kumfanya ajulikane, Keke alijiunga  na Joyous Celebration mwaka 2000-2001 akiwa miongoni mwa ma –solorist wa Kundi hilo linaloaminika kuwa is the most leading Gospel Group in Afrika. Akiwa na Joyous,  Keke ali-lead kwenye nyimbo iitwayo ‘Jo Ke Mohlolo-Hlolo’ (Joyous 6) kabla hajaondoka kundini humo. Baada ya kutoka Joyous Keke alifanya Kazi na wanamuziki wengi akiwemo Bheki Mseleku, Winston Mankunku na kundi la Umoja Choir.

Malkia wa Swazlland  alimuomba Keke atengeneze Live Recording Project chini ya Redemption Choir kitendo ambacho kilimpa keke nafasi ya kufanya kazi katika nchi jirani na Afrika ya Kusini hiyo ikiwa ni mwaka 2001-2004. Mwaka 2006 keke aliamua kuanza kufanya kazi zake binafsi. Album yake ya kwanza iliitwa “REVIVAL” ambayo ni LIVE DvD ilirekodiwa katika Chuo kikuu cha Ufundi cha Vaal cha nchini humo. Wakati akizindua album hiyo Keke alisema “Wakati umefika sasa kwa waafrika kuondokana na dhana ya kuwa Omba omba kwa kuwa tuna nafasi ya kupata kile tunacho kihitaji”

Keke na Mkewe Mphoza
Katika Maisha yake Keke husema hatosahau wakat aliporudi nyuma na kuachana na wokovu(backslide), alipitia maisha ya ulevi wa Pombe na madawa ya kulevya, ikafikia mahali akatengana na mkewe wa awali ambaye walijaliwa kupata watoto wawili Kganya (14) na Lesedi (10). Kwa sasa keke anaishi na watoto wake hao pamoja na bintiye aliyempata kutoka kwa mke wake wa sasa aitwaye Mphoza. Mpho kama waitavyo wao, kitaaluma amesomea masomo ya Uhandishi wa habari.

 Wakati mke wake Mpho alipokaribia kujifungua Mwaka jana mwanzoni keke aliwaambia waandishi wa habari kuwa  “This baby has brought us so much closer, To me it's a manifestation of my ability to be productive. Not just in this sense but in my ministry, in my music and even in business." Akaendelea kusema "I used to be stuck. Although my music was going well, the church wasn't growing. But now that's all changed. This little girl is a breakthrough. God is trusting us with this responsibility and a higher anointing."

Keke akiwa Uweponi kanisani kwake
Mafanikio ya album yake ya kwanza yalimpelekea Keke kufanya album ya pili iitwayo LIVING TESTIMONY,ya tatu inaitwa HOLLY OF HOLLIES na ya nne iliyotoka mwaka jana  2011 inaitwa “SPIRIT UNLIMITED”. Mafanikio ya album yake ya Pili iitwayo Living Testimony  ambayo ilifikia Platnum, yalionekana kuwashangaza watu wengi akiwemo keke mwenyewe. Katika Living testimony kuna nyimbo kama , I’m in love, I need your touch na Sefapano.

Keke akichukua moja ya Awards
Tofauti na Kuimba, Keke ni ni Mtumishi wa Mungu anayesimama katika Ofisi ya Kinabii, Prophet Keke  anaongoza kanisa liitwalo SHERKINAH GLORY WORSHIP TABERNACLE. Keke ni Baba wa watoto watatu na anaishi na kuhudumu na  Mkewe. Uwezo wake wa kuimba, kulimiliki jukwaa kwa namna ya pekee, pamoja na Kuhubiri kwa Nguvu kubwa za Roho mtakatifu ndivyo vitu vinavyomtofautisha sana Keke na Superstar yeyote umjuaye wa nyimbo za Injili Duniani.

Keke akiimba pamoja na Solly Mahlangu


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...