Tuesday, September 11, 2012

Don Moen Mwanamuziki wa injili anayewagusa wengi



Don moen ni muimbaji na mtunzi wa mashairi ya injili aliezaliwa tarehe 29 june 1950 huko Minneapolis Minnesota nchini Marekani. Don alifahamika baada ya kutoa album aliyoipa jina lake la Worship with Don Moen mwaka 1992. Album hiyo iliuza zaidi ya nakala milioni tano na kumfanya Don  kuwa kwenye orodha ya waimbaji waliouza zaidi nchini Marekani.

Don moen
Alifanya kazi na Integrity records kwa miaka 20 akiwa kama mbunifu mkuu wa integrity music na rais wa integrity lebel. Aliachana na integrity records mwaka jana(2008) na kuanzisha kampuni yake ya The Don Moen Company. Kampuni hiyo imempatia Don tuzo ya Dove mwaka huu huku akiwa na tuzo zingine tisa alizozipata kwa kazi ya muziki. Akiwa kama mtunzi wa mashairi amewatungia waimbaji wengi kama; Claire Cloninger, Paul Overstreet, Martin J. Nystrom, Randy Rothwell, Ron Kenoly, Bob Fitts, Debbye Graafsma, Paul Baloche na Tom Brooks.

Album ya Hossana give thanks ilikuwa album bora ya label ya intergrity, album hiyo ilifuatiwa na album nyingine mbili  zilizozofanya vizuri, En tu Presencia and Trono de Gracia ambazo alizitua kwa lugha ya kispaniola. Akiwa kwenye ziara barani Asia mwaka 1999 alirekodi singo ya The Mercy seat kwenye uwanja wa michezo wa Singapore nchini Malaysia na Heal our land akiwa Yodo park nchini Korea Kusini mwaka 2000.

God will give way(the best of don moen) ilitolewa mwaka 2003, wimbo uliobeba album hiyo wa God will give Way aliutoa maalum kwa ajili ya dada yake na mumewe ambao walimpoteza mtoto wao wa kwanza kwenye ajali mbaya ya gari huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya. Don anatarijiwa kutoa album ya I belive there is Way ambayo itakuwa ya mwisho kufanywa na Integrity records. Don ametoa Album zaidi ya album 20 baadhi ya album hizo ni;

.Give Thanks
. .Steadfast Love
.Bless the Lord
.Christmas
.Eternal God
.Worship with Don Moen
.God with Us
.Trust in the Lord – Live Worship with Don Moen
.Rivers of Joy
.Emmanuel Has Come
.Praise with Don Moen



TUZO

Baadhi ya tuzo alizoshinda nipamoja na hizi zifuatazo
Ameshinda tuzo za Dove mara tisa
1994-Album bora ya mwaka “God with Us”
Dove Awards
1992-Wimbo bora wa mwaka “God Will Make A Way”
1993-Album bora ya mwaka “Worship with Don Moen”
1995-Wimbo bora wa mwaka “Mighty Cross”
1998-Wimbo bora wa mwaka “Emmanuel Has Come”
1999 -Album bora ya mwaka “God for Us“
2001-Album bora ya kispaniola ya mwaka “En TĂș Presencia”
2003-Record bora ya country ya mwaka “God Is Good All The Time”
2004-Album bora ya kispaniola ya mwaka “Trono de Gracia”

Don kwa sasa anaishi Alabama nchini Maekani pamoja na mkewe Laura na watoto wao watano.


Monday, September 10, 2012

Picha Yetu Jumatatu Hii:John Lisu ndani ya City Christian Centre(CCC)

Pichani anaonekana mwanmuziki mahiri wa nyimbo za Injili nchini Mtumishi John Lisu akiimba huku akipiga galaton wakati wa Tamasha la kusifu na kuabudu lililoandaliwa na Vijana wa CASFETA mkoa wa Dar es salaam.Tamasha hili lilifanyikia katika kanisa la Upanga City Christian Centre(CCC) mnamo tarehe 1/09/2012.

Sunday, September 9, 2012

Sunday Sermon:Kwa Nini Mungu Anataka Watu Wake Wawe Matajiri?



Ile mwanzo 12:2 neno inasema “nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka”. Na Mwanzo 13:2 inasema“Naye Abramu alikuwa ni tajiri  kwa mifugo, na kwa dhahabu”.

Hapa tunaona jinsi Mungu anavyoweka ahadi ya kumbariki Abramu na kumfanya kuwa taifa kubwa. Kwenye sura ya 13 tunaona tayari Mungu ameshaanza kumbariki inasema alikuwa tajiri kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu. Bado katika 3Yohana 1:2 Mungu anasema “mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo .


Mpaka hapa tunaona kabisa ni mpango wa Mungu kutufanikisha katika mambo yote, hii ni pamoja na mafanikio ya kifedha. Na utajiri ambao Mungu anataka tuwe nao sio utajiri mdogo .Sasa swali ni kwamba kwa nini Mungu anataka tuwe matajiri? Maana kuwa tajiri bila kujua sababu za kuwa na huo utajiri utashindwa kujizuia kwenye matumizi mabovu ya huo utajiri (Fedha). Huenda zipo sababu nyingi, lakini mimi nataka nikuonyeshe sababu tatu za kibibilia.

Sababu ya kwanza , kulinda mawazo na mikakati ya Mungu kwa watu wake.
Yeremia 29:11. Mhubiri 7:12 “Kwa maana hekima ni ulinzi kama vile fedha ilivyo ulinzi na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliyo nayo” Mithali 18:11 “ Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake .
Kwenye kitabu cha Yeremia 29:11 

Mungu anasema nayajua mawazo ninayowawazia, si mawazo mabaya, ni mawazo ya amani ………..Sasa ukiunganisha mawazo ya mhubiri 7:12 na mithali 18:11 utupata sentensi hii. Mungu anapokupa utajiri (fedha), anakutajirisha ili kulinda mawazo (mipango) na mikakati ya Mungu ambayo anakupa kabla ya kukupa hizo pesa kwa watu wake. Fedha yoyote ambayo Mungu anaileta mikononi kwako kumbe ina makusudi, mipango ya Mungu ndani yake.


Mungu anayo mipango na njia za kuwafanikisha watu wake kiuchumi, kimwili, kibiashara, kimaisha  n.k. sasa hii mipango inalindwa na nguvu ya fedha. Maana kama watu wake watakuwa masikini basi mipango aliyo nayo juu ya kanisa, familia, nchi n.k. basi si tu haitatekelezeka vizuri bali pia itanunuliwa na shetani kwa fedha yake. Hii ina maana Mungu anataka tuwe na nguvu ya kimaamuzi na ya utawala kwa yale anayotuagiza Mungu kwa sababu kwa fedha.

Sababu ya pili , Ili kuliimarisha agano lake.
kumbukumbu 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili ALIFANYE imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Hapa tunaona wazi kabisa kwamba Mungu anasema ninakupa huo utajiri ili kulifanya agano lake kuwa Imara. Je agano hili ni lipi? Yeremia 31:31 inasema “Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, …. Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaindika; nami nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu wangu.

Agano ambalo Mungu anataka uimarishe kwa fedha anayokupa ni la yeye kukaa na watu wake. Maana yake tumia fedha anayokupa kujenga na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Yesu na watu wake.Uhusiano wa Yesu kama mwokozi, Rafiki, mpanyaji, Bwana n.k kwa watu wake maana yake ni hii, tumia fedha kufanya jambo lolote maadamu una hakika litapelekea uhusiano wa mtu (watu) na Yesu kuimarika na jina la Yesu kutukuzwa. Na kwa sababu hiyo utukufu wa mwisho wa nyumba hii/agano hili utakuwa ni mkuu kuliko ule wa kwanza, Hagai 2:8

Sababu ya tatu, ili tukopeshe na sio kukopa .
Kumbukumbu la Torati 28:12 inasema Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri … Nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe .Sikiliza tumeshaona katika mithali 18:11 kwamba mali ya mtu tajiri ni mji wake wenye nguvu… kwa lugha nyepesi maana yake fedha ya mtu tajiri ni nguvu ya huyo mtu kwenye mji aliopo/ au ambao yupo. Kwa kuwa akopaye ni mtumwa wake akopeshaye, hivyo utakapokopesha maana yeke utakuwa na nguvu juu ya maamuzi na hisia za huyo au hao watu uliowakopesha.

kama tukibakia kukopa tutakuwa watumwa na kwa sababu hiyo ndiyo maana Mungu anatupa utajiri kwa mtu mmoja, familia, kanisa, nchi n.k
Naamini sehemu ya kwanza ya somo hili litakusaidia katika matumizi ya utajiri ambao Bwana Mungu amekupa.

Na.Mwl Patric Sanga

Wachungaji wamtaka Rais Jakaya Kikwete achukue hatua


Rais Jakaya Kikwete
WACHUNGAJI wa makanisa ya kipentekoste wamemuomba Rais Jakaya Kikwete kuacha kuwa kimya wakati huu ambapo taifa lipo katika majonzi na badala yake achukue hatua ya kuwawajibisha viongozi wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kutokana na kushindwa kuiongoza wizara hiyo na kusababisha vifo vya raia wasio na hatia.

Wakizungumza jana na Tanzania Daima Jumapili, wachungaji hao walisema kuwa ni aibu kwa taifa ambalo limekuwa likihubiri amani na demokrasia likimwaga damu za watu wasiokuwa na hatia.

Mchungaji Onesmo Mwakyambo wa Kanisa la Agape RHEMA, lililopo mkoani Morogoro, alisema kuwa viongozi hao wameshindwa kujiwajibisha wao binafsi, hivyo kutokana na katiba kumpa mamlaka rais, anapaswa kuchukua hatua dhidi yao.
“Dhana ya uwajibikaji imeshindwa kufanyika hapa nchini hasa kwa viongozi wa sasa…tunakumbuka Rais wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliwajibika binafsi kutokana na kutokea kwa vifo, hivyo tunashangazwa na kitendo cha Waziri Emmanuel Nchimbi na naibu wake kuendelea kung’ang’ania madaraka,” alisema.

Alisema kuwa hatua ya kuendelea kulisifu taifa hili kuwa ni la amani haipaswi kuvumiliwa kwa kuwa polisi wamekuwa wakipindisha sheria kwa makusudi huku wakijiona kuwa wapo juu ya sheria.

Mchungaji Mwakyambo alisema kuwa hatua ya Rais Kikwete kuamua kuwa kimya na kushindwa kukemea vitendo hivyo sio tu kunajenga taswira mbaya kwa Watanzania bali pia hata yeye binafsi anachafuka kutokana na matukio hayo ya mauaji, likiwemo la mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni ya Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi aliyeuawa mkoani Iringa mwanzoni mwa wiki hii.

“Nchi hii haipo kwa ajili ya kundi fulani bali kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo hatua ya rais kushindwa kuzungumza neno juu ya matukio hayo jamii inamshangaa na haimwelewi hasa kutokana na yeye kuwa ndiye kiongozi mkuu wa serikali,” alisema.
Alisema serikali haiwezi kuwadanganya Watanzania katika mauaji hayo yanayoonekana kufanywa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya maslai ya watu wachache.

Huku akinukuu kifungu cha maandiko matakatifu ya Biblia Mithali 14:34 inayosema haki uinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote, alisema kuwa hatua ya kukaa kimya kwa Rais Kikwete inazidisha laana ndani nchi.Naye Mchungaji Isaack Kalenge, alisema kuwa hawapo tayari kuona taifa hili likiingia katika machafuko hivyo wanatarajia kuandaa kongamano la kuiombea nchi ili amani iliyodumu iendelee kuwepo.

Kalenge alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, kutumia hekima na busara katika kuongoza vyama hivyo la sivyo kauli zake zinaweza kuleta mvurugano zaidi miongoni mwa jamii.

Kutoka Magazeti ya Kikristo Jumapili hii kwa Ufupi


 
Gazeti la


Onyo: Kimbunga cha Katrina na Isaac ni Matokeo ya Uasi
Maangamizi makubwa yanayotokana na Vimbunga viwili vya Katrina na Isaac vilivyotofautiana miaka saba  imeeelezwa kuwa ni uharibifu uliotokana na hasira ya Mungu baada ya wanadamu kufanya matamasha makubwa ya Ushoga na uasi wa maadili uliopindukia.Watu hao walifanya sherehe kabambe ambayo ilijumuisha jumla ya watu 120,000 katika mji wa New Orleans sherehe hizo hufanyika baada ya miaka saba na ilibuniwa tangu mwaka 1972 na kukua taratibu.

Kikongwe mmoja mkazi wa eneo la New Orleans alisema hayo kufuatia kimbunga kutokea na kuwapiga, mji huo umekuwa mwenyeji wa sherehe hizo. kikongwe huyo aliongeza kuwa mi naona Mwisho unakaribia na uvumilivu wa Mungu juu ya Taifa la Marekani unafikia mwisho.


Jumapili ya Kihistoria ndani ya  Victory Christian Centre Tarbenacle(VCCT)
Kwa mara ya Kwanza kanisa la Victory Christian Centre Tarbenacle(VCCT) lililofahamika zamani kama Victory Christian Centre (VCC) limefanya ibada yao ya kwanza katika hema lao kubwa baada ya kuhamia rasmi.Kanisa hilo kwa sasa limehamia maeneo ya Mbezi Beach “A” na zamani lilikuwa katika ukumbi uliopo kituo cha Petroli cha Victoria jijini Dar es salaam.


Hema la Jipya la VCCT
Katika Ibada hiyo ya kipekee kila mtu aliinua sauti yake na kumtukuza mungu kwa ukuu na wema wake huku mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Dr Huruma Nkone alisema kuwa hayo ni matokeo ya baraka nyingi ambazo Mungu amewajalia kwa kununua kiwanja na kusimika hema la kuabudia lenye uwezo wa kubeba jumla ya watu zaidi ya 1000. Akitoa historia fupi ya kanisa hilo Dr Nkone alisema kanisa hilo lilianza mwaka 2005 na jumla ya watu 15 katika maeneo ya Muhimbili eneo la Scripture Union kisha likahamia katika ukumbi wa  kituo cha Petroli cha  Victoria na kwa sasa kanisa hilo lina zaidi ya washirika 1000.

Kanisa Lazindua siku 90 za Usomaji wa Biblia
Kanisa la TAG Changanyikeni Kizota jijini Dar es salaam limezindua siku 90 za kuchunguza maandiko ya Biblia ili waumini wake waweze kuwa imara katika kuisimamia Imani ya kweli ya Kristo Yesu, kama walivyofanya wana wa Beloya waliokuwa shupavu katika kuchambua maandiko.Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Mchungaji wa kanisa hilo Mch Emmanuel Sote alisema waumini wamekuwa wakisoma Biblia zao kama kawaida lakini la kusoma katika muda wa siku 90 zitaleta ari mpya ndani yao.

Mchungaji huyo amesema kuwa ingawa zoezi hilo litakuwa la miezi mitatu lakini kutafanyika zoezi la kufaya tathmini kuweza kujua wapi mtu hajaelewa au wapi panahitaji ufafanuzi ili mwisho wa zoezi hilo kila mtu aweze kutoka na kitu cha Ziada.

Ndondodoo Kutoka Jibu la Maisha
Zitto alia na uchache wa wataalamu wa gesi
Casfeta kuleta ukombozi kwa vijana
Ni nani ambao hawataonja umauti mpaka wauone kwanza ufalme wa Mungu?..(2)
Mungu anashughulika na Mavazi tunayovaa?


Gazeti la
Nyakati 
Gazeti huru la Kikristo la Kila wiki


Wanasayansi wadai Jua Kuzimika Dunia Nzima Dec 2012
Watafiti mahiri duniani wa mambo ya anga kutoka nchini Marekani(NASA) wanadaiwa kuchunguza na kubaini kuwa mnamo Desember 23-25 mwaka huu wa 2012 jua litazimika kama ilivyokuwa wakati Yesu anasulubiwa msalabani.Kama taarifa hiyo kutoka kwa NASA itakuwa ya kweli mabilioni ya watu watalazimika kusherehekea sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu(Christmass) wakiwa wangali gizani.

Kwa mijibu wa NASA Ndani ya siku hizo jua litashindwa kutoa Nuru yake na hivyo kutakuwa na giza totoro.Kwa mujibu wa wasanyansi hao ni kuwa dunia itahama kutoka hapo ilipo sasa ambapo kwa kipimo cha kisayansi kinaitwa “Three Dimension” na kwenda katika kipimo cha “Zero Dimension”.Wanasayansi hao wanadai katika kipindi hicho dunia nzima itakabiliwa na mabadiliko makubwa na hatimaye kutashuhudiwa dunia mpya kabisa ikiumbwa.

Bahati Bukuku Hajafa
Watu wasiofahamika na ambao malengo yao hayajafahamika juzi jumanne iliyopita(04/09/2012)  walieneza uvumi kuwa muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Bahati Bukuku kuwa amefariki dunia kwa ajali barabarani.Uvumi huo ulisambaasana kwa njia ya ujumbe mfupi na kituo kimoja cha redio nchini kilipiga simu katika chumba cha habari cha gazeti la Nyakati ili kujua kama habari hizo ni za Ukweli.

Bahati Bukuku
Baada ya taarifa hizo gazeti la Nyakati lilifanya utafiti na hatimaye lilipata nafasi ya kuongea na Bahati Bukuku mwenyewe na kuthibitisha kuwa yuko hai na muda huo alikuwa maeneo ya Mabibo studio akirekodi video ya album yake ya mpya iitwayo Dunia Haina Huruma.

Askofu ahoji Wazinzi kutengwa wasiotoa zaka kuachwa
Askofu wa kanisa la International Evangelism Sinai askofu Silvester Thadei amewataka watumishi wa Mungu kuacha kabisa kukemea na kuchagua dhambi za kukemea na kutenga waumini pindi wanapokiuka misingi ya Kiroho.Askofu Thadei huchunga kanisa la “Mlima wa Bwana”  lililoko Ipagala mjini Dodoma, askofu huyo  aliyasema hayo wakati akihubiri kanisani hapo jumapili iliyopita.

Akitoa mfano askofu huyo alihoji  mantiki ya baadhi ya viongozi wa dini kukemea na kuwatenga waumini waliofanya dhambi ya Uzinzi huku wakiwaacha bila kuwakemea waumini wasiomtolea Mungu fungu la Kumi. Ikiwa wote hao( wazinzi na wasiomtolea Mungu fungu la kumi) wote wamemkosea Mungu kuna sababu gani ya watumishi wa Mungu kukemea dhambi moja na nyingine kuachwa bila kuchukuliwa hatua stahili alihoji askofu Dhadei.

Jenipher Mgendi kutoa Filamu Kuiponya Jamii
Muimbaji wa nyimbo za Injili na muaandaaji wa filamu za kikristo nchini mtumishi Jenipher Mgendi amekamilisha Filamu nyingine iitwayo CHAI MOTO.Hii ni filamu ya nne kutoka kwa mwanamama huyo  ikitanguliwa na Joto la Roho,Teke la Mama, pamoja na Pigo la Faraja.Mgendi ameliambia gazeti la Nyakati kuwa filamu hiyo ni ya dakika 115 na kwa sasa tayari ipo madukani.

Jenipher Mgendi
 Kwa mujibu wa Mgendi filamu hiyo inazungumzia changamoto mbalimbali zilizopo katika maisha ya ndoa na hasa pale wanandoa wasipompatia Mungu nafasi ipasayo.Filamu hiyo imeongozwa na Christian Mhegga na Mgeni Hamisi huku wahusika wakiwa ni Jenipher Mgendi mwenyewe, Musa Banzi, Juma Mtima, Christine Matai,Yvyone Cheryl maarufu kama monalisa na wasanii wengine wengi.

Ndondoo kutoka Gazeti la Nyakati
Nabii apinga kuombea Adui
Wasio na mafanikio hawalijui Neno
FPCT Sombetini Arusha kupanua eneo lao
Jaji Warioba - Waacheni wanachi wachangie Maoni yao juu ya katiba

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...