Friday, June 3, 2011

Imani sio Kumlazimisha Mungu kufanya Tunavyotaka

Mwl Silvester Gamanywa
Bila shaka umewahi kusikia kauli kama  hizi, Nitamuomba Mungu lazima anifanyie Muujiza., au Lazima Mungu anifanyie a, b, c. Hili Neno lazima linapoelekezwa kwa Mungu  kwanza ni Kumvunjia Heshima yake. Ni sawa na Kumuamuru Mungu afanye mapenzi yetu, badala ya sisikufanya Mapenzi ya Mungu.Kwa hiyo kauli za Kumlazimisha Mungu kujibu maombi ni Utovu wa Nidhamu mbele zake.



Aidha ni lazima tujue kwamba imani sio kitu cha kumshinikiza Mungu kuwa ni lazima!, lazima!, lazima!!! Hata kama tutanukuu vifungu vya maandiko na kuvifanya kama kigezo cha kumshinikiza Mungu ili afanye vile tunavyoomba.Ukweli unabaki pale pale  kwamba Mungu hatekelezi amri ya kiumbe wake.



Nasisitiza katika hili maana siku hizi jamii yetu imejaa waumini wengi wenye utovu wa Nidhamu wa hali ya juu kiasi cha kumwamrisha Mungu ajibu maombi yao, tena kwa jinsi wanavyotaka wao. Na pengine wengine wao huenda Mungu aliwahi kuwajibu Maombi yao pindi walipokuwa bado wachanga kiimani(Kiroho). Lakini wao wakadhani ndio mtindo wenyewe kumfokea na Kumgombeza Mungu ili ajibu Maombi yao.



Ndugu zangu pamoja na kwamba Mungu huchukuliana na udhaifu wetu, lazima tujue hii huwa ni kwa Muda kitambo, na anao ukomo wa kuchukuliana na ujinga na uchanga wetu.

Mwl Silvester Gamanywa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...