Wednesday, June 29, 2011

Nguvu ya Maombi - Pastor Ibra Munanka


BWANA YESU asifiwe mpendwa!
Nakukaribisha katika ukurasa huu tena ili tujifunze maana ya maombi. hili neno "maombi" si neno geni miongoni mwa wakristo au wasio wakristo.Kwa haraka haraka tunaweza kusema, maombi yanafanywa na mhitaji au mtu aliyegundua kuwa amepungukiwa! na hapo inaonesha kuwa anahitaji msaada!

Miongoni mwa wanadamu, karibu kila mtu hujiona amepungukiwa, hata yule anayefikiri amefanikiwa sana, ahitaji msaada wowote, bado anajihisi amepungukiwa akubali au akatae. ndio maana kila mtu bado anataka kwenda kazini, hata kama bado anaonekana nazo pesa nyingi kiasi gani. 

vile vile kila mtu amepungukiwa, kwani hakuna mtu anayeishi bila kuhitaji huduma kadha wa kadha, hauwezi kukaa eneo moja ulilo lala au kukaa ama kusimama wiki au mwezi mzima, lazima utahitaji kuamka, kusogea. na pia huwezi tu uka kaa kimya kipindi chote, lazima utatamani kuzungumza na wengine. Bwana Yesu Kristo anasema "nyinyi hamwezi neno lolote" (Yohana 15:5b).
 
 Mambo muhimu ya kuangalia 
Ni vyema tuelewe kuwa, si wanadamu wamepanga kuomba, ila ni Mungu ndie anayepanga na kuwa na kiu kuwa sisi wanadamu twende mbele zake kuomba. Tazama Isaya 1:18=20, Mungu anasema " Haya njoni tusemezane..Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya". 

Mpendwa wangu, kwa maneno hayo tunaona kuwa maombi ni mazungumzo, mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu. Yeye (Mungu), anasema, na mwanadamu anasema, wote katika hali ya kusikilizana.

Cha kujiuliza hapa, Siku za leo, wanadamu wengi tunapoingia kwenye maombi, ni sisi tu  tunapokuwa ktk maombi, mara nyingi huwa tunamwambia Mungu mahitaji yetu au kumshukuru! Je, huwa tunamsikia na yeye akijibu au kuzungumza au kutueleza mambo kadha wa kadha? kama sivyo ni kwa nini hatumsikii?

Tuonane wakati mwingine tena!
Pastor Ibra Munanka
+255713714453
Tanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...