Tuesday, June 21, 2011

Lazima uisome Hii: Mahakama ya Ulaya yaingilia kati kuhusiana na Haki za wakristo


Serikali ya Uingereza imeambiwa iweke bayana kuhusu kama haki za wakristo na ukristo zimewekwa kando na Mahakama ya sasa ya nchi hiyo. Ombi hilo limeombwa na Mahakama ya haki za binadamu barani Ulaya katika mji wa Strasbourg kwa niaba ya wakristo wane ambao wameadhibiwa kutokana na kuonyesha imani zao kwenye vituo vyao vya kazi.


Wakristo hao wameamua kwenda kwenye mahakama ya Bara la ulaya kutokana na rufani yao ya kupinga kuadhibiwa kutupwa mbali na mahakama ya Uingereza. Wakristo hao wa kwanza ni Nadia Ewedia ambaye yeye ni mfanyakazi wa shirika la ndege la Uingereza(British Airways), Nadia alipigwa marufuku kuvaa msalaba kwenye sare zake za kazi.

Kituo cha sheria cha Kikristo nchini Uingereza(Christian Legal Centre) kimeamua kuwasaidia wakristo wawili ambao nao wameadhibiwa na mahakama ya nchini Uingereza. Wakristo hao Gary McFarlane na Shirley Chaspin kila mmoja amekutwa na masahibu tofauti.

Gary McFarlane ambaye ni mshauri wa mambo ya Mahusiano ambaye alifukuzwa kazi kutokana na kugoma kutoa ushauri kwa ndoa ya mashoga ambao walikuja kwake kutaka ushauri. Shirley Chaspin ambaye kitaaluma ni nesi , yeye alifukuzwa kazi  kwa kuwa alikatazwa kuingia kwenye wodi za hospitali aliyokuwa akifanyia kazi huku akiwa amevaa mkufu shingoni(necklace) wenye alama ya Msalaba. Baada ya kugoma kuvua msalaba shingoni Shirley aliondolea kazini.

Mtu wa nne ni msajili wa  wa zamani wa ndoa ambaye aliadhibiwa na Baraza la Kaskazini la jiji la  London mara baada ya kukataa kufungisha ndoa ya jinsia moja.

Mkurugenzi wa kituo cha sheria cha kikristo Bw Andrea Minichiello Williams amesema  “inaonekana wazi kuwa mahakama ya uingereza haiitendei haki imani ya kikiristo, kama ombi letu kupitia mahakama ya bara la ulaya likifanikiwa, hii itabadilisha hali nzima iliyopo na kuwapa uhuru wakristo kwenye vituo vyao vya kazi”

Mapema mwaka huu mahakama ya Ulaya iliiruhusu nchi ya Italia kuendelea kuweka alama ya msalaba kwenye madarasa ya shule za nchi hiyo mara baada ya mabishano makali kisheria kati ya wanasheria wa nchi hiyo na wale wa mzazi mmoja mmama aliyekuwa akidai uwepo wa misalaba madalasani unaondoa haki yake ya kumfundisha mwanae kuhusu Imani ya mwelekeo mwingine tofauti na ukristo.


Source: Christian Post 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...