Tuesday, June 7, 2011

Mchungaji wa kipentekoste akili kunywa kikombe cha Babu

Mchungaji Focus Komba anayeendesha huduma yake katika eneo la Bunju B  jijini Dar es salaam amejitokeza wazi na kukiri kuwa amekunywa kikombe cha Babu.Mchungaji komba ni mchungaji wa kwanza toka madhehebu ya kipentekoste hapa nchini anayekiri wazi kuwa ameenda Samunge na kupokea kokombe. Kumekuwa na malumbano Mengi hususani kwa wakristo juu ya uhalali katika Mungu juu ya  matumizi ya kikombe cha babu.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi, Mchungaji komba alisema utoaji wa sadaka na fungu la kumi hauleti baraka kwa muumini kama ambavyo wachungaji wengi wanasisitiza. Badala yake Baraka zinawafuata watu wote wenye kwenda zaidi ya hapo na kutoa fungu la ishirini, yaani asilimia ishirini ya kipato chao.Anadai fungu la kumi lilihubiriwa wakati wa Agano la Kale na sio katika agano Jipya.

Mch Komba anasema  mkristo anapotoa fungu la kumi anakuwa tayari ameshapata kile alichotolea fungu la kumi yaani tayari anacho ndio maana kakitolea fungu la Kumi.Lakini  atoapo fungu la ishirini anakuwa amemshawishi Mungu kumzidishia baraka. Anasema wakristo wanakosa Baraka kwa sababu wanapokea kiasi kinacholingana na utoaji wao, na hivyo kuwaacha wachungaji wakifaidi mafungu ya kumi wakati wao wakiwa na hali mbaya kiuchumi na hawajui wamekosea wapi.

Aidha Mch Komba anasema Yesu mwenyewe alipokuja katika Agano jipya hakueleza habari za Fungu la kumi ,bali zaidi ya Fungu la kumi.Alinukuu kwenye Mathayo 5:20 na 2Nyakati 31:5-10 tunaona wana wa israeli walivyomtolea Mungu Dhaka na Malimbuko na Mungu akawabariki.

Na:Theonestina Willbard

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...