Saturday, June 25, 2011

Usijisumbue wala kuhangaika katika kufanya uamuzi wowote

Mwl Christopher.Mwakasege akiwa madhabahuni akifanya huduma
Katika kufanya maamuzi mazuri maishani, ni vizuri kuwa makini mno kwa kuwa uamuzi wowowte utakaouchukua ni mbegu, na mbegu hiyo unaipanda kwa kuufanyia kazi uamuzi huo. Hivyo usiwe na uamuzi ambao hauko tayari kuvuna kutokana na matokeo hayo.

Katika maisha kuna maamuzi mengi ambayo huambatana na mahangaiko na usumbufu mwingi ndani ya MOYO wa mtu.Lakini maamuzi mengine huwa hayana mahangaiko wala usumbufu, na kwa sababu hiyo unajikuta unayanya kirahisi.

Usije  ukaingia kwenye mtego wa kuona maamuzi yaliyo magumu ndio ya kumshirikisha Mungu pekee, nay ale yaliyo mepesi ndiyo unayoyaamua bila kumshirikisha Mungu. Neno la Mungu linatuambia hivi “ Msijisumbue kwa neon lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba,pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane kwa Mungu.” ( Wafilipi 4:6).

Yesu Kristo aliwahi kusema Hivi, “…..pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote”(Yohana 15:5). Hii inamaana ni pamoja na kufanya maamuzi!. Hatuwezi kufanya maamuzi mazuri pasipo msaada  na Uongozi wa bwana Yesu.

Ndiyo maana tunaambiwa hivi”Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake, huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha na mambo yenu” ( 1Petro 5:6-7)

Hebu linganisha maneno hayo na haya ya Mithali 3:5,6 yanayosema “ Mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako mkiri yeye, naye atanyoosha mapito yako”

Ukijua haya utajizoesha  kumwomba Mungu kila siku ili aongoze maisha yako, kwa maneno Mengine utakuwa na maana ya kwamba unataka aongoze maamuzi yako. kumbuka maisha ya mtu ni mtiririko wa maamuzi yake mwenyewe naya watu wengine.

Mwl C.Mwakasege

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...