Tuesday, June 21, 2011

Historia ya Mwanauziki wa Injili K` Basil

Kashumba Basil (K` Basil)
Basil Kashumba ni Kijana aliyezaliwa Mwaka 1978 Mkoani Kagera katika wilaya ya Bukoba, toka kipindi akiwa mdogo alikuwa akipenda sana muziki na tofauti na wanamuziki wengine pamoja na kupenda sana Muziki aliyamudu vyema masomo yake darasani.

Bidii yake kimasomo ilimfikisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UD) ambako alihitimu shahada ya Jiografia na Mazingira. Akiwa chuoni  UD ndipo alijijengea jina kubwa kupitia muziki wa Duniani(Circular Music). Watanzania wengi wamefanikiwa kumfahamu vizuri K Basil mara baada ya kutoa nyimbo yake ya Riziki aaakiwa na Mwanadada Stara Thomas ambaye naye kwa sasa inaaminika kuwa ameyakabidhi maisha yake kwa Kristo.

Stara Thomas naye inaaminika kwa sasa ameokoka
Pamoja na mafanikio aliyokuwa nayo kwa kipindi chote hicho, K Basil anasema maisha yake yalitawaliwa na na taabu nyingi. Pombe ndio ilikuwa rafiki mkubwa na kiongozi wa K Basil. “Nilijaribu kuacha Pombe lakini ilishindikana, nilkuwa mlevi kupindukia na mara nyingi nililala Bar mpaka nikawa kero kwa Rafiki zangu.”

Achilia mbali ulevi na uzinzi anasema siku moja akiwa amelewa aliwahikupata ajali mbaya ya gari, na katika aliwahi kutupwa jela mara kadhaa kutokana na mikasa ya hapa na pale.” Nimepitia misukosuko mingi nay a Ajabu lakini sasa  nimekuwa mtu huru, mwenye amani, upendo na Faraja kutokana na kumtegemea Mungu”

Katika vurugu zangu zote hizo “siku moja nikasikia Sauti ndani yangu ikiniambia yanipasa nibadilike, niliamua kumshirikisha dada yangu kile nilichokiskia toka ndani na nikamwambia kuwa nahitaji kuombewa. Niliamua kwenda kanisani ambako niliongozwa sala ya toba  na huo ukawa mwanzo wa safari yangu mpya ya maisha”

Kwa sasa ninafanya Kazi ya Mungu kwa Moyo mmoja na ninaendelea na huduma ya uimbaji, ninamshukuru Mungu kwa mafundisho niliyopata kupitia kwa Mchungaji wangu Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ maarufu kwa jina la Ufufuo na Uzima lililoko kawe jijini Dar es salaam.

Basil anasema baada ya kumrudia Mungu na kusimama imara katika wokovu n wakati wake mwafaka kuwarudisha kwa kristo watu wengine waliopotea katika ulimwengu wa anasa na dhambi kama ilivyokuwa kwake. Hivi sasa amezindua album yake iitwayo “YESU ANANIPENDA” yenye jumla ya nyimbo kumi zikiwemo Namjua, wakatina bahati, Wewe ni Baba, Rudisha, Utukuzwe, Moyo, Tunasonga Mbele, Mama na Ahsante Yesu iliyobeba jina la album.

Tarehe 5/12/2010 Basil alifunga ndoa na Perida Mdegela ambaye wanaishi naye kwa furaha mpaka hivi leo. Anasema anamshukuru Mungu kwa kuwa kwa sasa akili imetulia. Aidha Basil alipoulizwa anazungumzia vipi wokovu wa Mwanamuziki Stara Thomas Basil anasema “Kwa hakika hizi ni Habari Njema ingawa sijui ni nini kilichomuongoza, nafikiri kuungana naye tena kufanya nyimbo ya Injili”.
Basil akiwa na mkewe Pelida Mdegela
 Kwa sasa Basil ni mmoja wa wachungaji katika kanisa la Glory of Christ akimtumikia Mungu chini ya Askofu Gwajima. Hosanna Inc inamtakia kila la Heri  Basil kwenye safari yake ya wokovu tukiamini Basil ni moja kati ya vitendea kazi katika ufalme wa Mungu kwa ajili ya Kuujenga na Kuuimarisha Mwili wa Kristo hapa Tanzania na duniani kwa ujuma.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...