Saturday, June 11, 2011

Mkurugnzi wa Manispaa ya Iringa akataa watu kuwasaidia watoto wa mitaani


Wiki hii mkoani Iringa mkurugenzi wa Manispaa hiyo ametoa waraka unaowakataza wasamaria wema kuwapa pesa watoto wa mitaani. Tamko hili limekuja mara baada ya kuonekana kuwa watoto hao wanapopata pesa hujisahau na kuona ndio mfumo wa maisha kwa kuwa wanapokuwa makwao hawapati fursa ya kupata pesa kama wakiwa mtaani, hivyo kwa namna moja au nyingine pesa hizo huwa kama urimbo wa wao kuendlea kukaa mtaani na kuomba omba.

Kibiblia, pamoja na tamko la mkurugenzi huyo tunaona wajibu wa kanisa juu ya watoto hao. Jambo hili linabaki kuwa changamoto sio tu kwa serikali bali hata kwa kanisa kwa kuwa kanisa lina mchango wake juu ya watoto hao. Swali linakuja Je? kanisa linafanya wajibu wake juu ya watoto hao au nalo linaungana na Mkurugnzi wa manispaa ya Iringa?.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...