Monday, June 13, 2011

Kanisa La EAGT Laendesha Mikutano Mikubwa ya Injili Dar- es salaam na Mwanza

Askofu Dr Moses Kulola
Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) linaenesha mikutano mikubwa ya injili katika majiji ya Dar es salaam na Mwanza. Mikutano hiyo imeanza kwa pamoja leo jumapili na inatarajia kumalizika tarehe 19/06/2011 yaani jumapili ijayo.

Katika mkutano wa Dar es salaam huu unafanyika katika viwanja vya Jangwani ambapo askofu mkuu wa Kanisa hilo Dr Moses Kulola atakuwa akihubiri na kufanya maombezi kwa watu wenye shida mbalimbali. Katika mkutano huo wa Jangwani wanamuziki Mahiri toka nchini Kenya Solomon Mukubwa na Anastazia Mukabwa wataungana na magwiji wa Muziki wa injili nchini Bony Mwaitege na Frola Mbasha katika kumpatia Mungu utukufu


Mkutano wa Injili wa Eagt Unaoendelea hivi sasa katika eneo la Nyakato jijini Mwanza

Katika mkutano wa injili wa Mwanza huu unafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nundu iliyoko wilayani Ilemela katika kata ya Nyakato. Mkutano huu wa Mwanza umeandaliwa na kanisa la EAGT Buzuruga Mwanza chini ya Mchungaji Saimon.Vikundi mbali mbali vya uimbaji vimealikwa katika kuhubiri injili katika viwanja hivyo.


Kanisa la EAGT ni moja kati ya makanisa machache nchini yenye kuratibu mikutano ya nje ya injili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...