Nisher |
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. kwa muda sasa Nisher amekuwa akijihusisha na muziki(Gospel and Non Gospel Music),toka mwaka huu uwanze ndoto yake ya kuwa na studio kubwa kwa ajili ya kurekodia aina zote za Muziki imekamilika na sasa anamiliki studio ijulikanayo kama NISHER RECORDS iliyoko jijini Arusha.
Kipekee nimeanza kumfahamu Nisher takribani miaka mitatu iliyopita nikiwa mwaka wa pili chuoni pale St Augustine Univ, na hii ni baada ya kuona quality ya Video production ya Ziara na huduma za Nabii Geordavie,nilipouliza who is behind this unique art nikaambiwa ni mwanaye anaitwa Nisher.Unaweza mjudge Nisher vyovyote but pamoja na hayo Nisher is Talented, hufanya Graphics za viwango vya juu kuanzia Video mpaka Photo Pictures
Baada ya studio yake kuanza kazi studio jijini Arusha huku ikigharimu Kwa haraka haraka zaidi ya 15M inadeal na Video na AUDIO,kwa kutambua mchango wa Baba yake katika maisha yake na katika mafanikio yake Nisher aliamua kurekodi Mini Video Clip kwa ajili ya kumshukuru baba yake kwa hatua aliyomfikisha. Katika Video Clip hiyo, Nisher anasema mafanikio yake yote yanatokana na baba yake.
Nisher akiwa ndani ya Nisher Records |
Katika Maisha ya wokovu,watu wengi waliookoka huwa wako mstari wa mbele katika kukosoa na kulaunu namna watoto wa watumishi wanavyoishi na namna wanavyouchukulia wokovu.Kwa upande wa pili kanisa linasahau wajibu wake kwa vijana na kubaki kuwalaumu na kuwafanya ndio Hot topic popote pale hususani wanapotoka nje ya mstari.Pamoja na yote hayo Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kuwa Habadiriki, na kanisa lapaswa kusimama na kuwaombea watumishi pamoja na familia zao pasipo kuwanena vibaya.