Tuesday, June 12, 2012

Askofu atishiwa kuuawa


Askofu Edson Mwombeki wa kanisa la Tanzania Evangalism Field (TEF) la mjini Shinyanga ametishiwa kuuwawa kutokana na kuelezwa kuwa anashirikina na vikongwe anao walea  wapatao 23 kwa  lengo la kufanya nao ushirikina kwa kuwatoa maeneo ya vijijini na kuwaleta mjini kuwaweka kambi na kuwapatia chakula,malazi na mavazi.

Askofu Edson Mwombeki akiwa na mmoja wa mabibi anaowatunza

Watu hao  watano alionaswa majina yao kwa kumfuata eneo la kanisani kwake na kumtishia maisha aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa mara kwa mara amekuwa akitishiwa maisha na kuyapuuzia sasa imefikia hatua ya watu hao kufika mwisho

Alisema alitishiwa kuuwawa kutokana na kutuhumiwa kuwa anawalea vikongwe hao ambao ni wachawi na kushirikiana nao kwani wanamuundia njama ya kumuua pamoja na vikongwe hao ambao anawalea kwenye kambi iliyoko kolandoto manispaa ya mjini hapa .

“Mmoja wa wahusika hao ambaye anajulikana  kwa jina la Saidi Seleman alifika hapa  kanisani na kuanza kutoa matusi kisha kunza ugomvi na mtoto Mrokozi (7) baada ya kumpiga alianza kulia ndipo mimi nilipomuuliza kijana huyo na kuanza kutoa lugha chafu za matusi na kudai kuwa nitakuua na hao  vikongwe vyako kwani hatufahamu kuwa unashirikiana nao kwa mambo ya kishirikina”alisema

Kutokana na hali hiyo aliamua kutoa taarifa katika jeshi la polisi kwa kitendo hicho na kuwaeleza maneno yaliyosemwa hata kipindi cha nyuma vijana wengine wanne wakiwa na huyo saidi walikwisha sema maneno hayo hivyo lisemwalo lipo naona kwanza nijisalimishe kwenye jeshi  halafu apambane nao kikamilifu.

Washirika wa  kanisa la Tanzania Evangalism Field (TEF) la mjini Shinyanga wakiwa ibadani
Alisema amekuwa akijitolea pesa kwa kuwasaidia jamii ambayo inamaisha magumu kama walemavu,Albino na vikongwe wakiwemo watoto yatima na wenye kuishi na virus vya ukimwi mkoani hapa bali yeye hana lengo baya kama jamii inavyomfikilia hao anawafananisha na mashetani walio muasi  mungu kwa mawazo mabaya kwake.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa  Evarist Mangalla alithibitisha kutokea kwa vitendo hivyo vya vitisho na suala hilo analifuatilia kwa ukaribu ili kufahamu watu hao wanalengo gani kwa askofu huyo ikiwa pia tayari kijana mmoja amekwisha kamatwa  na  sasa yuko nje kwa mdhamana.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...