Thursday, June 21, 2012

Stand Up Gospel Comedy ndani ya City Christian Centre jumapili hii


The King of Stand up Gospel Comedy in Tanzania Prezo Chavala akiwa katika moja ya harakati on stage
Baada ya kufanya Tamasha la KUCHEKA TENA la mwisho pale Landmark Hotel,Ubungo mwezi wa tatu na hatimaye Arusha mwanzoni mwa June hatimaye mkali na muasisi wa christian comedy nchini Tanzania anatua tena jijini Dar es salaam kwa Tamasha lake la nne toka ameanza mwishoni mwa mwaka jana pale Ubungo plaza.

Yaani ni kucheka na kucheka na kucheka tena huku ukimsifu Mungu na kujifunza yapasayo kutenda katika maisha yako ya utauwa.Tamasha hili litawasimamisha Up Coming Comedians wa kutosha katika segment maalum ya OPEN MIC, na wale ambao wamezoeleka kama Richard Chidundo,Gerald Mrema,Josephine na wengine watakuwa sambamba na waimbaji kama

Sarah Shila,
Deogratius, Meshack,
Gee & Seth,
WordAlive
Dar es salaam Gospel Bands,
Golden Eagles and
1st Q dance groups

Tamasha Hilo Litaanza Saa 9:00jion-1:30 Usiku
Ukumbi:City Christian Centre(CCC)
Kiingilio 5000/=
Na 2000/= Tu Kwa Watoto.

Katika SERIES hii bado tuko Msimu(SEASON) wa kwanza na hili Tamasha lijalo litakuwa Tamasha la tatu kwa Dar es salaam  na ni Episode II. Kama ilivyotaarifiwa mapema Tamasha hili la jpili ijayo(24th June 2012) pamoja na mawili yafuatayo kwa hapa Dar(Yaani Tar 23th Sept na 23/30th Novemba-mkesha wa mwisho) yatafanyika katikaukumbi wa CITY CHRISTIAN CENTRE-UPANGA(Mkabala na Mzumbe Dsm)

Tamasha Hili Limedhaminiwa na Great Potentials Ltd,City Christian Centre(Ccc),TouchingVision,Author2readers,Wordalive Church,Olympus Computers And Chavala Ideas Platform.

Sehemu ya umati uliohudhuria Night of Transformation usiku ambao uliandaliwa jijini Arusha na Prezo Chavala
Akielezea mafanikio yaliyopatikana Chavala amesema “Kwa kweli mafanikio ni makubwa sana mpaka sasa ingawa mengine hayawezi kuonekana kwa macho ya nyama ila itoshe tu kusema mafanikio ni makubwa mno;yaani toka kule ambako nilikuwa sitambuliki na watu kwa makusudi walikuwa hawataki kuona umuhimu wa Comedy katika ulimwengu wa kikristo mpaka sasa ambako wengi wameanza kuelewa, wamepokea na wamekubali.

kibali nilichokipata Arusha kwa mfano ni kikubwa mno kiasi cha kushangaza; kwa sasa nina vijana wengi sana ambao wamevutwa na kuona nao wanaweza kumtumikia Mungu kwa vipaji vyao kama vile Comedy,Dance na Mashairi na mengine mengi ya vipaji halisi, hivyo nina wanafunzi wakutosha na zaidi washika dau,wachangiaji na wanaounga mkono ni wengi sana na hata wewe unaesoma hapa unakaribishwa kuwa mmoja wao.

Hosana Inc itakuwepo katika onyesho hili na kukujuza LIVE kila kitachojiri 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...