Sunday, June 10, 2012

Mzee Makasy,Stara Thomas,Cosmas Chidumule wa hudumu katika Tamasha la kuiombea Amani Tanazania

John Shabaani
Jumapili ya leo tarehe 08.06.2012 hapa katika kanisa la TAG Magomeni jioni hii kunafanyika tamasha la kusifu na kuabudu ambalo limeandaliwa na mtumishi wa Mungu John Shabaani .Katika tamasha hili mgeni rasmi ni Waziri wa habari vijana utamaduni na watoto Mh Dr Fenella Mukangara.Mh Mukangara ameongoza harambee ya kuchangia huduma ya mtumishio wa Mungu John Shabaani.

Moja kati ya matukio muhimu katika tamasha hili linaloendelea hapa ni uwepo wa wakongwe wa injili nchini Mzee makasi pamoja na Mzee Cosmas Chidumule.Pamoja na hayo Upendo Kilahilo, John Shabaani pamoja na Apostle John Komanya walipanda jukwaani na kuimba kwa pamoja wimbo wa tenzi uitwao KALE NILITEMBEA  amabao kimsingi umegusa mioyo ya wengi.Katika tamasha hili rangi iliyotawala ni Red kama ionekanavyo pichani na limehudhuriwa na Rais wa waimbaji nchini Mtumishi Addo November.

Stara Thomas akienda sawa na Cosmas Chidumule


Bishop John Komanya , Upendo Kilahiro na John Shabaani awakiimba

John Shabaani akiwa anahudumu

Sehemu ya umati

Hawa ni back up team ya john Shabaani

Sifa zikiendelea

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...