Sunday, June 24, 2012

Kutoka Magazeti ya Kikristo Jumapili hii kwa Ufupi


Gazeti la

Mtawa aibuka na Tiba ya Ukimwi Mlimani
Mamia ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa sasa wanamiminika katika kilele cha Mlima Pima ulioko wilayani Rolya Mkoani Mara kwa ajili ya kunyweshwa dawa inayotibu magonjwa sugu ikiwemo na ukimwi,dawa hiyo inatolewa na mtawa wa kanisa katoriki ajulikanaye kama Martha Magdalena Nyangwe anayedai kuoteshwa.Mwandishi wa gazeti la Jibu la Maisha alilazimika kupanda mpaka kileleni alipo mtawa huyo ili kujionea ukweli wa mambo.

Mwandishi wa Jibu la Maisha baada ya safari ndefu alifanikiwa kufika kileleni mwa mlima huo unaokadiriwa kuwa ni mita 400 kutoka usawa wa ardhi.Mwandishi alipomuuliza mtawa huyo dawa hiyo ameitoa wapi alijibiwa  ameoteshwa na bikira Maria(mama wa Yesu) ambaye alimwambia atumie visima viwili vilivyochongwa na Mungu Mwenyewe kuwaokoa wanadamu wanaoteseka na magonjwa.Bi Nyangwe ni mtawa wa shirika la Lejo-Maria lenye asili yake nchini Kenya.

Pindi mtu anapokaribia katika eneo hilo huamriwa kuvua viatu kwa kuwa eneo hilo ni takatifu,mgonjwa hutakiwa kupiga magoti chini, Bi nywangwe huchota maji kwenye kisima kwa kutumia kibuyu kilichokatwa na kuyaweka pembeni, kisha huchukua mkia wa N’gombe na kuuchovya kwenye dawa ya kufukuzia mapepo ili kumuandaa mgonjwa kunywa dawa.Wakati huo wasaidizi wa mtawa wakiwa kama kumi wakiimba nyimbo za kumsifu Bikira Maria, kisha Bi Nyangwe humywesha dawa mgonjwa pasipo kufuata vipimo.

Tahadhari:Katika siku hizi za Mwisho Mengi yametokea na yatatokea, ni Vizuri kama kanisa litasimama katika nafasi yake na kuchambua kulingana na maandiko pasipo kupelekwa pelekwa.


Wainjilisti wasomewa dua ya mauti Lindi
Timu ya wainjilisti kutoka Dar es Salaam wamesomewa dua ya mauti mkoani Lindi na wakasimama katika kumtetea YESU na mwisho wa siku Yesu akajitolea utukufu.Timu hiyo  ya wainjilisti na waimbaji ilitoka jijini Dar es Salaam katika kanisa la TAG Ubungo ambao kwa pamoja walipiga kambi wilayani RUHANGWA mkoani Lindi kwa lengo la kuhubiri injili kwa wiki moja.

Kwa mujibu wa mmoja wa wainjilisti hao Mtumishi Francis Mulinda amesema wenyeji wa eneo hilo walionyesha wazi kukerwa na uwepo wao mahali hapo.Watumishi hao walikuwa na desturi ya kuomba kuanzia alfajiri mpaka saa nne asubuhi kisha kwenda kwenye uinjilisti wa nyumba kwa nyumba.Inadaiwa siku ya kwanza wakati wapishi wakiendelea na kazi yao mara alikuja kijana na kushika kitabu cha dini ya mama mdogo kisha kuanza kukisoma, wao hawakujali kisha wakaendelea na kazi zao.

Kesho yake asubuhi baaada ya maombi alikuja mtu akawauliza Je mko salama? tukamjibu ndiyo akasisitiza ni kweli mko wazima tukamjibu ndiyo.Baadaye walikuja watu wengine kama wanne nao wakaanza kusoma kitabu chao kwa muda kisha wakaondoka.Lakini pamoja na hayo yote timu nzima iliondoka Lindi ikiwa salama huku watu wengi wakifunguliwa akiwemo Bi Habiba ambaye alikuwa ameolewa na jini kwa muda mrefu.


Baraza la Maaskofu wa kipentekoste lasema MIHADHARA inamkera Mungu
Baraza la maaskofu wa  kipentekoste nchini PCT,limeitaka serikali ipige marufuku mihadhara yote inayoendelea nchini kwa kuwa imekuwa chanzo cha vurugu zote zinazotokea kwa sasa hapa nchini.Akizungumza na Jibu la Maisha makamu mwenyekiti wa baraza hilo Askofu Daniel Aweti amesema, serikali inapaswa kupiga marufuku mihadhara yote kwa lengo la kupunguza majanga yasiyo ya lazima.


Gazeti la
Nyakati


Mchungaji asema manabii wengi wanaogopa kashfa
Mchungaji David Mpanji wa jijini Mbeya amesema wapo wachungaji wengi wenye karama za Kinabii lakini hawajitamulishi kama manabii kwa kuogopa kashfa zinazotolewa na watu mbalimbali kuwa hakuna nabii wa Mungu katika dunia hii.Mchungaji huyo amezidi kusema wachungaji hao wanaoogopa kasha wanapaswa kutambua kuwa kukashifiwa ni sehemu ya kupakwa mafuta.

Kwa kuanzia amesema yeye mwenyewe amewahi kukutana na kashfa hizo lakini tangu akutane na kashfa hizo amemuona Mungu kupita kiasi.


Askofu Irene Nzwalla mjane anayehudumia wajane
Katika gazeti la Nyakati safu ya Uso kwa Uso na Mtumishi wako jumapili hii yupo Askofu Irene Nzwala wa kanisa la Hosanna Christian Centre Mision lenye makao yake makuu jijini Mwanza.Mama Irene Nzwala ni mwinjiristi na amekuwa akifanya mikutano ya nje kwa muda mrefu sasa.Mama Nzwala amekumbana na vikwazo vingi katika utumishi wake ikiwa ni pamoja na wengine kupinga kitendo cha mwanamke kuwa askofu au mchungaji ila kwa Neema ya Mungu amelishinda hilo.

Mama Nzwala aliwekewa mikono ya kuwa Askofu mkuu wa Hossana Christian Centre na Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of GOD Tanzania(EAGT) Askofu Moses kulola miaka kadhaa iliyopita.Kupitia kanisa la Hossana Christian Centre mama Nzwala mabaye pia ni mjane amekuwa akitoa msaada kwa wajane na watoto yatima.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...