Thursday, June 14, 2012

KAPOTIVE STAR SINGERS – BUKOBA


Kapotive Star Singers Kutoka Bukoba
KAPOTIVE Star Singers kutoka Bukoba Tanzania, ni kikundi kilichoanzishwa mwaka 2009, kikiwa na lengo la kueneza neno la Mungu kwa njia ya nyimbo za injili.

Kikundi hiki kinaundwa na waimbaji nane, wachezaji sita na wapiga vyombo wanne. Kikundi kinaongozwa na Mwl. Alexander Ndibalema – Mkurugenzi, Andrew Kagya – Mratibu, Theresia Kagya – Katibu, Claudius Mutabuzi – Mhasibu, Audax Mathias – Afisa masoko na Denis Deus – Afisa mahusiano. Na huduma zote za kitumishi wanafanyia wilayani  Bukoba mkoani  Kagera nchini Tanzania.

Tangu kuanzishwa kwake, kikundi kimeshatoa albums tano amabzo ni
Yesu ni Mwema
Zawadi ya Krismass
Naitamani Mbingu
Mama yetu
Asante Baba

Kapotive Star Singers

Mpaka sasa album yao ya kwanza yaani “YESU NI MWEMA” ndio imefanyiwa video, na nyingine maandalizi yanaendelea ili kuweza kuzifanyia video.

Unaweza kuona baadhi ya shughuli zetu kwenye youtube (youtubekapotive), facebook (Kapotive Singers) na Twitter (kapotivestarsin).

Kwa mawasiliano zaidi: simu +255 752 - 360213, +255 754 – 511552 au +255 784 – 263891.Email:kapotive@yahoo.com


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...