Gazeti
la
Mtawa aibuka na Tiba ya Ukimwi Mlimani
Mamia
ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa sasa wanamiminika katika kilele cha Mlima
Pima ulioko wilayani Rolya Mkoani Mara kwa ajili ya kunyweshwa dawa inayotibu
magonjwa sugu ikiwemo na ukimwi,dawa hiyo inatolewa na mtawa wa kanisa katoriki
ajulikanaye kama Martha Magdalena Nyangwe anayedai kuoteshwa.Mwandishi wa
gazeti la Jibu la Maisha alilazimika kupanda mpaka kileleni alipo mtawa huyo
ili kujionea ukweli wa mambo.
Mwandishi
wa Jibu la Maisha baada ya safari ndefu alifanikiwa kufika kileleni mwa mlima
huo unaokadiriwa kuwa ni mita 400 kutoka usawa wa ardhi.Mwandishi alipomuuliza
mtawa huyo dawa hiyo ameitoa wapi alijibiwa ameoteshwa na bikira Maria(mama wa Yesu)
ambaye alimwambia atumie visima viwili vilivyochongwa na Mungu Mwenyewe kuwaokoa
wanadamu wanaoteseka na magonjwa.Bi Nyangwe ni mtawa wa shirika la Lejo-Maria
lenye asili yake nchini Kenya.
Pindi
mtu anapokaribia katika eneo hilo huamriwa kuvua viatu kwa kuwa eneo hilo ni
takatifu,mgonjwa hutakiwa kupiga magoti chini, Bi nywangwe huchota maji kwenye
kisima kwa kutumia kibuyu kilichokatwa na kuyaweka pembeni, kisha huchukua mkia
wa N’gombe na kuuchovya kwenye dawa ya kufukuzia mapepo ili kumuandaa mgonjwa
kunywa dawa.Wakati huo wasaidizi wa mtawa wakiwa kama kumi wakiimba nyimbo za
kumsifu Bikira Maria, kisha Bi Nyangwe humywesha dawa mgonjwa pasipo kufuata
vipimo.
Tahadhari:Katika
siku hizi za Mwisho Mengi yametokea na yatatokea, ni Vizuri kama kanisa
litasimama katika nafasi yake na kuchambua kulingana na maandiko pasipo
kupelekwa pelekwa.
Wainjilisti wasomewa dua ya mauti Lindi
Timu
ya wainjilisti kutoka Dar es Salaam wamesomewa dua ya mauti mkoani Lindi na
wakasimama katika kumtetea YESU na mwisho wa siku Yesu akajitolea utukufu.Timu
hiyo ya wainjilisti na waimbaji ilitoka
jijini Dar es Salaam katika kanisa la TAG Ubungo ambao kwa pamoja walipiga
kambi wilayani RUHANGWA mkoani Lindi kwa lengo la kuhubiri injili kwa wiki
moja.
Kwa
mujibu wa mmoja wa wainjilisti hao Mtumishi Francis Mulinda amesema wenyeji wa
eneo hilo walionyesha wazi kukerwa na uwepo wao mahali hapo.Watumishi hao
walikuwa na desturi ya kuomba kuanzia alfajiri mpaka saa nne asubuhi kisha
kwenda kwenye uinjilisti wa nyumba kwa nyumba.Inadaiwa siku ya kwanza wakati
wapishi wakiendelea na kazi yao mara alikuja kijana na kushika kitabu cha dini
ya mama mdogo kisha kuanza kukisoma, wao hawakujali kisha wakaendelea na kazi
zao.
Kesho
yake asubuhi baaada ya maombi alikuja mtu akawauliza Je mko salama? tukamjibu
ndiyo akasisitiza ni kweli mko wazima tukamjibu ndiyo.Baadaye walikuja watu
wengine kama wanne nao wakaanza kusoma kitabu chao kwa muda kisha
wakaondoka.Lakini pamoja na hayo yote timu nzima iliondoka Lindi ikiwa salama
huku watu wengi wakifunguliwa akiwemo Bi Habiba ambaye alikuwa ameolewa na jini
kwa muda mrefu.
Baraza la Maaskofu wa kipentekoste lasema MIHADHARA inamkera
Mungu
Baraza
la maaskofu wa kipentekoste nchini
PCT,limeitaka serikali ipige marufuku mihadhara yote inayoendelea nchini kwa
kuwa imekuwa chanzo cha vurugu zote zinazotokea kwa sasa hapa
nchini.Akizungumza na Jibu la Maisha makamu mwenyekiti wa baraza hilo Askofu
Daniel Aweti amesema, serikali inapaswa kupiga marufuku mihadhara yote kwa
lengo la kupunguza majanga yasiyo ya lazima.
Gazeti la
Nyakati
Mchungaji asema manabii wengi wanaogopa kashfa
Mchungaji
David Mpanji wa jijini Mbeya amesema wapo wachungaji wengi wenye karama za
Kinabii lakini hawajitamulishi kama manabii kwa kuogopa kashfa zinazotolewa na
watu mbalimbali kuwa hakuna nabii wa Mungu katika dunia hii.Mchungaji huyo
amezidi kusema wachungaji hao wanaoogopa kasha wanapaswa kutambua kuwa
kukashifiwa ni sehemu ya kupakwa mafuta.
Kwa
kuanzia amesema yeye mwenyewe amewahi kukutana na kashfa hizo lakini tangu
akutane na kashfa hizo amemuona Mungu kupita kiasi.
Askofu Irene Nzwalla mjane anayehudumia wajane
Katika
gazeti la Nyakati safu ya Uso kwa Uso na
Mtumishi wako jumapili hii yupo Askofu
Irene Nzwala wa kanisa la Hosanna Christian Centre Mision lenye makao yake
makuu jijini Mwanza.Mama Irene Nzwala ni mwinjiristi na amekuwa akifanya
mikutano ya nje kwa muda mrefu sasa.Mama Nzwala amekumbana na vikwazo vingi
katika utumishi wake ikiwa ni pamoja na wengine kupinga kitendo cha mwanamke
kuwa askofu au mchungaji ila kwa Neema ya Mungu amelishinda hilo.
Mama
Nzwala aliwekewa mikono ya kuwa Askofu mkuu wa Hossana Christian Centre na
Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assemblies of GOD Tanzania(EAGT) Askofu Moses
kulola miaka kadhaa iliyopita.Kupitia kanisa la Hossana Christian Centre mama
Nzwala mabaye pia ni mjane amekuwa akitoa msaada kwa wajane na watoto yatima.