Monday, January 2, 2012

Changers Conference 2012Mwanza International Community Church{MICC} chini ya Pastor Zakayo Nzogele imeandaa kongamano maalumu kwa ajili ya wanavyuo wote wa jijini Mwanza. Kongamano hilo la kipekee litafanyika katika ukumbi wa Nyumbani Hotel ambapo MICC Praise Team itakuwepo ukumbini hapo kuongoza sifa na kuabudu. Kongamano hili linatarajia kufanyika siku ya Tarehe  12/01/2012 kuanzia saa 3: 00 Asubuhi mpaka saa 12:30 jioni.

Katika kongamano hilo lililopewa jina la CHANGERS CONFERENCE linalengo hasa kuwa-train vijana kuwa chachu ya mabadiliko katika nyanja zote kwa manufaa ya nchi yetu ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla. Pamoja na kwamba target kubwa imewekwa kwa Vijana wote walio vyuoni, pia kongamano hili ni darasa huru kwa wote hata ambao sio wanavyuo wenye lengo la kuleta Mabadiliko na Theme ya Kongamano hilo ni “CATALYST OF CHANGE” 

Kuna Msemao wa wenzetu unasema “When You Don`t Travel You May See Your Mom is a Best Cooker “, some times tunapoanza Mwaka huu wa 2012 unaweza amini kuwa Mipango uliyonayo inajitosheleza, iko Vizuri na Itakutoa Laaa!!, usiishie hapo, kama kijana ulio kanda ya ziwa fika tarehe 12/01/2012  pale Nyumbani hotel ili upate Elimu ya Ziada kutoka kwa watumishi wa Mungu itakayokupa Mwanga zaidi katika kutimiza ndoto zako kwa Mabadiliko ya nchi yetu.

Wasemaji wakuu katika Kongamano hilo watakuwa ni Pastor Zakayo Nzogelle ambaye ni Senior Pastor wa MICC pamoja na Mr Daniel Mikenze ambaye ni Managing Director wa EFFCO(PYT) LTD. Kiingilio katika Kongamano hilo ni sh 3000 kwa kila atakayehudhuria ambayo ndani yake utapata Chakula standard(Lunch) pamoja na Usafiri kutoka chuoni kwako mpaka ukumbini. Maelezo ya kina yatatolewa kwa wale wote wenye lengo la kwenda kusoma nje ya nchi.

Tiket Zinapatikana katika Campus Zote 

Bugando University – Maria Kipele 0713-521118
CBE – Samwel (Tafes Vice Chairperson) 0652-926649
Saint Augustine University (SAUT) – Barnabas Shija 0717-642263 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...