Monday, January 30, 2012

Dr Mwakyembe Amshukuru Mungu Baada ya Kupona


Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika jana kanisani hapo.
Dk. Harrison Mwakyembe alifika kanisani hapo na kutoa  ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa miujiza yake.

Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo kisha akamkaribisha Dk Harrison Mwakyembe
Dr Mwakyembe aliongozana na wabunge kadhaa kwenda kanisani hapo akiwemo Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta,kwa upande wake Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla.

Source:John Bukuku

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...