Wednesday, January 25, 2012

Uwepo wa Mungu Watawala katika kongamano la Wanafunzi wa Sekondari jijini MwanzaMnamo tarehe 21 jan 2012 Blog  hii ya Hosanna Inc kwa kushirikiana na Mtumishi Jackson Mndeme kutoka Dar es salaam, Pastor Isaack Obed wa Mwanza pamoja na Mtumish Willbert Pantaleo wa MOI University(Nairobi) tuliandaa Kongamano la lililowahusisha wanafunzi wa shule za sekondari zilizoko jijini Mwanza na lilifanyikia katika shule ya sekondari Mwanza(Mwanza Sec). 

Haikuwa kazi nyepesi ila kwa msaada mkubwa wa MUNGU alilifanikisha jambo hili kwa utukufu wake na  kwa ushirikiano wa viongozi wa vikundi vya dini kutoka  UKWATA, CASFETA, TYCS, pamoja na  ASA.

Mtumishi Jackson Mndeme kutoka Dar es salaam ndiye aliyekuwa mnenaji mkuu wa kongamano hilo na alifundisha ujumbe wa neno la Mungu wenye kichwa cha habari kisemacho “MAWAZO YA MUNGU JUU YETU”. Baada ya mafundisho hayo mtumishi wa Mungu mndeme pamoja na Pastor Isaack walifanya maombezi kwa wanafunzi wa kidato cha sita ambao wanatarajia kuanza kunza mitihani yao ya Mwisho (NECTA) tar 8-02-2012. Pamoja na kwamba tulichelewa kumaliza hadi kwenye saa nane mchana lakini bado watu walikuwepo wakimsifu Mungu baada ya maombezi yote kumalizika.

Baada ya Maombezi kwa form six kulifanyika maombezi kwa wanafunzi waliokata shauri kumpokea YESU kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao baada ya kuongozwa sala ya toba, kisha yakafuata maombezi wa wanafunzi wote wenye shida na mahitaji mbalimbali na uwepo wa MUNGU ulikutana na haja zao. 

Shukrani za pekee ziende kwa Praise and Worship Team kutoka Saint Augustine University(TAFES) na kanisa la Devine Favour kwa kuhakikisha kazi ya Mungu inafanyika kwa ufasaha mahali pale. Sifa na Utukufu ni kwa MUNGU PEKEE na Hakika Tumemuona Bwana akifanya Mengi makubwa tofauti na tulivyofikiria.

Sehemu ya Musician wakiwa On Stage

Praise ikiendelea

Praise Team ikihudumu


Utukufu apewe Bwana, aliyepokea Mamlakaaa, asifiwe Bwana YESU Mile.....

Willbert kutoka Victory Christian Centre akihudumu

Mtumishi Jackson Mndeme akifundisha katika kongamano hilo

Wanafunzi wakisikiliza NENO la MUNGU

Baada ya NEN0 Maombezi yalianza

His hand is not short that it can not rescue

Pastor Isaack Obed akifanya Maombezi
Wahudumu wakielekea Prayers room

Maombezi yakiendelea

Minister Mndeme akifanya Maombezikuna watu wanaitwa Colours of the Events, huwezi wakosa kwenye any Event, katikati ni BroAdolph Nzwalla, akiwa na Ruth Lyanga Kulia na kushoto ni Vicky Bonge huyu kuanzia Sifa Zivume pale mlimani city,RIOT, Changers Conference na nyingine nyingi bonge huyu ndani.Mwishoni Praise and Worship iliendelea, angalia hii Video Clip Sister Ruth Lyanga akilead Katikati ya Wafalme Hakuna Mungu kama wewe


4 comments:

 1. This is Awesome job u guys conducted. May Heavenly Father bless u all : )

  ReplyDelete
 2. SO UPLIFTING,GOD BLESS U ALL FOR TAKING PRECIOUS TIME TO CHANGE YOUTH GENERATION FOR THE GOD.KEEP IT UP

  ReplyDelete
 3. I once felt that I should be a part of all this. I'm so sorry that I couldn't. Hongereni watumishi kwa kazi nzuri ya Mungu.
  > Ben Bravo 'Junior

  ReplyDelete
 4. Naaaaaaaaaaam!
  To God be the Glory!Thats how we Christian Youth should be!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...