Monday, January 9, 2012

ThanksGiving Concert In MwanzaJumapili ya jana tarehe 08-Jan-2012 katika kanisa la FPCT Kitangiri Mwanza kulifanyika Tamasha maalumu la kusifu na kuabudu. Tamasha hilo lililokuwa na lengo la Kumshukuru Mungu kwa kutufikisha mwaka 2012 liliandaliwa na Bro Samuel Batenzi. Hapo awali Tamasha hili lilipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Nyumbani Hotel lakini kutokana na tatizo la Kiutawala kati wamiliki wa jengo(NSSF) na Nyumbani Hotel wakiwa kama wapangaji, tamasha hili lilihamishiwa katika kanisa la FPCT lililoko Kitangiri jijini Mwanza.

Tamasha hilo liliongozwa na Samwel Batenzi pamoja na Praise team iliyowahusisha waimbaji kadhaa kutoka makanisa tofauti jijini Mwanza. Moja kati ya vitu vya kufurahisha katika uandaaji wa Tamasha hilo ni kwamba 95% ya waandaaji na waimbaji walikuwa ni Vijana ambao ki-umri sio wakubwa sana bali walidhamiria kumshukuru Mungu kwa pamoja 

Barnabas Shija kutoka Saint Augustine University aliongoza shughui hiyo akiwa kama Mc. Miongoni mwa watu waliohudhuria Tamasha hilo ni Pamoja na Askofu Mkuu wa FPCT Tanzania.

Samwel Batenzi on Stage 

Praise team

Samwel Batenzi na Ruth Lyanga wakihudumu

Glory Be To GOD

Bro Ihano Nestory na Adolph Nzwala wakiabudu
 
Shangwe kwa Mungu wetu

Born again Modo "Felix mshama” kushoto akienda sawa na Imma with
White wristband


Chini ni Bro Adolph Nzwalla akilead Ahsante Yesu

4 comments:

 1. Dhu Mpe hi Ihano, sikuwa najua kabisa Kamanda Adolf kuwa ni Mtu wa Kipaza, Mwambie Wajina Samuel Batenzi nimempa salute kendeleza fun....Huyu Born Again Modo a.k.a BOM nikija mwanza utanionesha aiseee

  ReplyDelete
 2. Hongereni sana. Samwel Mungu akubariki na kukuongeza katika huduma hii. Mungu apanue hozi yako. Mbarikiwe sana.

  ReplyDelete
 3. Papaa@asante kaka,kwa utukufu wa Mungu,majina haya ya Samwel lazima yejenge ufalme wa Mungu kwa kiwango cha juu sana

  ReplyDelete
 4. Chatawe@Asante sana Pastor,utukufu urudi kwa yule aliyeweka hiki ndani yangu

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...