Wednesday, January 18, 2012

Hosanna Inc Tour to Mwanza Secondary


Hosanna Inc Blog kwa kushirikiana na Bro Pataleo willbard, Jackson Mdeme pamoja na Mchungaji Isaack Obed tunawakaribisha wanafunzi wote wa shule za sekondari zilizopo Jijini Mwanza katika Kongamano maalumu la wanafunzi wa sekondari litakalofanyika katika shule ya Sekondari Mwanza siku ya Jumamosi ya tarehe 21-01-2012 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa saba mchana.
Lengo kubwa la kongamano hilo ni kuwafundisha na kuwahimiza wanafunzi wa sekondari jijini Mwanza kuzidi kumtumikia MUNGU katika ujana wao na katika MASOMO yao kwa Mwaka 2012. Msemaji mkuu katika Kongamano hilo ni mtumishi wa MUNGU JACKSON MNDEME kutoka jijini Dar es salaam pamoja na Bro Pantaleo Wilbard kutoka MOI University(Nairobi) pamoja na Mtumishi Isaack Obed wa jijini Mwanza.
Mpaka sasa maandalizi yameshakamilika ikiwa ni Pamoja Mtumishi Mndeme,pamoja na Pantaleo  tayari wako jijini MWANZA. Kongamano hili litakuwa ni Kongamano la kwanza kufanyika jijini MWANZA ambalo litawaweka pamoja wanafunzi wa shule zote za sekondari jijini MWANZA kutoka vikundi vyote vya dini kuanzia UKWATA, CASFETA,HUIMA, TYCS, pamoja na ASSA. kwa upande wa uimbaji Praise and Worship team kutoka TAFES SAUT pamoja na Divine Favour watahudumu, Watu wote wanakaribishwa WAGONJWA NA WENYE SHIDA MBALIMBALI WATAKUTANA NA NGUVU ZA MUNGU.

Mtumishi Jackson Mndeme akihudumu katika Fellowship ya Mwanza sekondari siku leo jumatano, baada ya hapo tulielekea Bwiru GirlsMtumishi Jackson Mndeme akitoka kuongea na wanafunzi wa Mwanza Sekondari kama Sehemu ya maandalizi ya kongamano la Jumamosi


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...