Sunday, January 8, 2012

Christina Shusho Tena


Christina Shusho
Kwa muda mrefu sasa media nyingi za Tanzania zimekuwa zikiplay nyimbo za kundi la Christ Ambassadors Choir. Album ya kundi hilo kutoka Kigali Rwanda  iliyopewa jina la KWETU PAZURI (Video na Audio) kwa takribani miezi mitano  toka August 2011 imekuwa ikisikika sio tu kwenye media bali hata majumbani, mitaani na sehemu mbalimbali. Kitendo cha Christina shusho kuingiza sokoni album yake ya VIDEO iitwayo NIPE MACHO mnamo tarehe  tarehe 23/dec/2011 imeonekana kuteka hisia za wengi kwa utukufu wa Mungu.

Katika Video Album hiyo ya Shusho iliyofanywa tena na kampuni ya MBC HOTMEDIA, nyimbo ya kuabudu iitwayo NATAKA USHIRIKA NA WEWE ndiyo inayoongoza kuchezwa katika media mbalimbali ambapo jumapili iliyopita ya tar 1jan 2011 nyimbo hiyo pamoja na Nyingine iitwayo NINA WIMBO zilichezwa kwa mara ya kwanza na katika kituo acha Television ya CITIZEN cha nchini Kenya katika kipindi cha RAUKA Kinachotayariswha na K-KREW.

Wakati Christina Shushu ameuanza Mwaka huu wa 2012 kwa kishindo kwa album yake hiyo ya Video, nguli mwingine wa Muziki wa injili nchini ROSE MUHANDO na yeye Mwaka huu wa 2012 anatarajia kuingiza sokoni album yake ya Video iitwayo” UTAMU WA YESU” baada ya ile ya Audio aliyoitoa mapema mwaka jana. Kufanya Vizuri kwa Video album hii ya NIPE MACHO ni hatua ya kwanza kabla hajaachia Video album yake nyingine iitwayo KWA KANISA LA KRISTO.1 comment:

  1. Christina kama mtumishi wa Mungu nakupa ushauri- kwanza uwe natural kama ulivyokuwa hapo mwanzo. unamuimbia Mungu na si w/damu, fanya shooting zako katika uhalisia ili mtu akitaka kuabudu aingie rohoni si kutazama mara uko hotel mara kwenye maji n.k.usivae hayo manywele yasiyo yako kisha ukamsifu/ kumwabudu bwana. rudi kama mwanzo, ulikuwa asilia, na ukapendwa, utauona mkono wa Bwana
    Mt. Glory Giliard..........

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...