Sunday, January 29, 2012

Kauli za watumishi wa MUNGU Kwenye Mitandao Jamii wiki hii

 Kutoka mtandao wa Twitter
Pastor Rick Warren

 
Rick Warren
Today, be the living expression of Jesus' kindness to everyone - with your words, smile, eyes, & hands.

Bishop jamalbryant


The people who are mad about what you've achieved.....have no power to stop what you are destined to accomplish!

CeCe Winans


It's time to go higher in God!!! Let's elevate our minds so that we can continue to give God more. He wants our best!!!


Kutoka mtandao wa Facebook

   

Bishop TD Jakes

‎Forgiveness is a BIG idea! It takes a person who thinks big ideas, rather than comparatively small thoughts, to introduce and practice forgiveness effectively. God saw the grand scheme of things and knew it was going to take an equally grand plan of forgiveness to bring each of us back to Himself. Have you accepted God’s BIG idea?

Pastor Isaac Malonga


"Do not try to Imitate what God is doing, before you Imitate His Heart" - Bishop Tumwidike”.

Dada Mary Damian-Strictly Gospel


  

Mary Damian
Mwaka mpya umeshaanza na maisha yanaendelea...hekima ya Mungu ikawe juu yetu kutambua fursa zitakazotokea...ni wakati wa kufanya maamuzi, kuyaendea maono na kuifanya kila siku iwe nzuri...Nawatakia heri wandugu!


 Mada kutoka Facebook Group la wajoli

                         

"Mnaposali msipayuke payuke ili watu wawasikie........"Je ni sawa kusali kwa sauti tunapokusanyika kufanya maombi tena wengine sauti ya kupayuka kabisa?kwa nini kila mtu asisali kimoyomoyo bila kutoa sauti ?Top of Form
Emmanuel Ivan Msamba ULOKOLE NI UFARISAYO MAMBO LEO!


Emmanuel Destiny Man Huu nao ni uchanga wa kiroho.
Emmanuel Ivan Msamba ‎.1 Samuel 3:7-11
7 Now Samuel did not yet know the LORD: The word of the LORD had not yet been revealed to him.

8 A third time the LORD called, “Samuel!” And Samuel got up and went to Eli and said, “Here I am; you called me.”

Then Eli realized that the LORD was calling the boy. 9 So Eli told Samuel, “Go and lie down, and if he calls you, say, ‘Speak, LORD, for your servant is listening.’” So Samuel went and lay down in his place. .

Denn'o Franco kupayuka ni kuongea maneno yasiyo na maana, sio kuomba kwa sauti


Denn'o Franco kuna faida kadhaa kwanini tunaomba kwa sauti, kwanza, kuzuia interfereance ya vitu vingine kwenye maombi yako. Pia kama ujuavyo shetani hapendi watu waombe ukifanikiwa kushinda kuomba kila siku zaidi ya saa2 basi umetoboa wengi hawawezi, hivyo shetani huleta usingizi. ukiomba kimya kimya waweza jikuta umelala. na hata hukumbuki ulikuwa unaomba


Mgisa Mtebe ‎"Msipayuke-payuke" katika sala na maombi haimaanisihi "sauti kubwa" mpendwa! Ni udhaifu wa Kiswahili tu ndo unaotugonganisha hapa. Soma msatari huo katika kiingereza utaona jinsi watafsiri wanavyoweza kupotosha kanisa. King James Version Bible ametumia neno "Vain Repititions" yaani Kurudia-rudia Maneno bila maana na mpangilio. Bible nyingine ya Kiingereza imetumia Neno "Bubbling" yaani kulipuka-lipuka au kuropoka-ropoka, ikiwa na maana kutamkatamka maneno bila mpangilio unaoleta maana. Ila Waswahili waliotafsiri Bible enzi ile, walikosa msamiati sahihi, au ni wa madhehebu yasiyokubaliana na kusali kwa sauti, hivyo yamkini wali-intend kuipotezea kwa style hiyo.

Tunapokwenda mbele za Mungu, tunatakiwa tujipange kifikra ili uwe na maneno yenye maana na mtiririko mzuri hata kama unasali kimya-kimya au unasali kwa sauti. Somo la Yesu ktk mistari hii halikuhusu sauti, kwani hata Yesu mwenyewe alikuwa anasali kwa sauti na kwa machozi mpaka ikabidi awe anakwenda mlimani, ili kupata utulivu lakini pia ni ili asisumbue majirani (Waebrania 5:7) "Yeye (Yesu) katika siku za mwili wake, alimtolea (Mungu) ... maombi na dua na kulia sana na machozi." Siku ya Pentekoste, Roho aliposhuka kwa kanisa, Kanisa lilipuka kwa maombi ya pamoja na sauti kuu ikasikika mji mzima, kutoka katika kile chumba cha ghorofa. Fikiria sauti iliyowakusanya watu wa mji mzima, ni sauti kubwa kiasi gani. (Matendo 2:1-4). "...wakampazia Bwana sauti zao..." katika maombi (Matendo 4:24).

I stand to be corrected!

Emmanuel Ivan Msamba Mhhh! Denn'o Franco! Uliwahi kusoma sehemu yoyote iliyoonyesha kuwa waumini wa kanisa la mwanzo enzi za mitume walisali kama tunavyopayuka walokole siku hizi? Kama ni kwa sauti ni kwa nini basi asisali mmoja baada ya mwingine? Iko wapi ile 'NENA BWANA MTUMISHI WAKO ANASIKIA?'
Mgisa Mtebe Baada ya kusoma maelekezo hayo hapo chini, utagundua kwamba, ni lazima mtu anapotaka kwenda mbele za Mungu, ajiandae kifikra na kujipanga kumweleza Baba haja za moyo wake. Usiende mbele za Mungu na kuanza kuongea bila kufikiri. Ndio maana Mhubiri 5:1-2 "Jitunze mguu wako unapokwenda mbele za Mungu, usiwe na maneno mengi, kwasababu Yeye ni Mfalme wako na yuko juu. Ni bora uende kusikia kuliko kutoa kafara ya kipumbavu (maelezo yamefafanuliwa)". Kafara ni sadaka. Na sadaka zi lazima ile tuliyozoea. Kuna sadaka za maneno (Biblia inaita, 'dhabihu' za sifa). So usiende mbele za Mungu kuongea bila kujipanga.

Nadhani utakuwa umeshawasikia watu waliomzoea Mungu na waliozoea sana kuongea na Mungu kwa kuropoka, ni wale wanaosali asubuhi lakini katika maneno yake kwa Mungu, anajikuta amesema "Baba tunakuja mbele zako jioni ya leo" ingawa time hizo ni asubuhi. Hiyo ndio kuropoka. Ni kuongea kwa mazoea, bila kufikiri.Ndio maana Mhubiri 5:1-2 "Jitunze mguu wako unapokwenda mbele za Mungu, usiwe na maneno mengi, kwasababu Yeye ni Mfalme wako na yuko juu. Ni bora uende kusikia kuliko kutoa kafara ya kipumbavu (maelezo yamefafanuliwa)".


1 comment:

  1. KAKA YANGU MGISHA YOUR OKY KWA SABABUKUSALI NI ZAIDI YA KUTAMKA NA KUTOA MAELEZO HAUYA NI MAOMBI UNATYO YA PELEKA MBELE ZA MUNGU KWA MALENGOKAMILI

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...