Tuesday, January 24, 2012

Sir Andy Chande Mtanzania wa Kwanza kukiri wazi kuwa ni Mwanachama wa Freemason


Sir Andy Chande

  ~ “Nilipoanza kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambua kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na dunia.”

 ~ Asema “Nina hati “takatifu” ya kuhani mkuu freemason”

~ kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ilianzishwa Zanzibar mwaka 1904

Sir Andy Chande ni mtanzania wa kwanza kukiri kuwa ni mwanachama wa kundi la Freemasons, Chande tofauti na kuwa member wa kundi hilo pia anakiri kuwa ameshika nyadhifa nyingi ndani ya kundi hili ikiwa ni pamoja na kutunukiwa hati takatifu ya Kuhani Mkuu. Katika maelezo yake pia ametaja asasi zilizofadhiliwa na kundi hilo lililoenea duniani kote.

Maisha yake kama mwanachama wa kundi hilo ameyaweka katika kkitabu chake Katika alichokiita  SHUJAA KATIKA AFRIKA, safari kutoka Bukene, Mzee Chande ni Mtanzania aliyewahi kushika nyazifa mbali mbali katika utumishi wa umma katika Serikali ya Tanzania  na kujizolea sifa kadhaa ikiwa ni pamoja na Heshima ya “Sir” aliyopewa na Malkia wa Uingereza. Katika kitabu hicho ameeleza kwa kina jinsi alivyoingia katika chama hicho Oktoba 25, mwaka 1954, akianzia na kambi inayoitwa Jaha iliyomaanisha kundi la watu wa daraja la nne.

Kati ya mwaka 1967 na 2003 Sir Andy Chande amekuwa mwenyekiti wa Tanzania Tourist Corporation, Tanganyika Standard Newspapers Ltd, East African Harbours Corporation, East African Railways Corporation and Cargo Handling Company of East Africa ltd.Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika mashariki Sir Chande alikuwa mwenyekiti wa Air Tanzania Corporation na baadaye akafanya kazi kama Mwenyekiti Mamlaka ya Bandari Tanzania na pia Mwenyekiti wa Tanzania Railways Corporation.

Katika Ukurasa wa 168 wa kitabu hiki kilichozinduliwa kwa heshima na viongozi wa wakuu wa serikali ya Tanzania, Sir Chande anasema:


Jengo la Freemasons lililoko maeneo ya Posta jijini Dar es salaam
“Kuwa mwanachama wa Freemason maana yake ni mtu kujitolea kuingia katika safari ndefu isiyo na mwisho ya kujifunza na kuchunguza. Kwa muda wa miaka 50 iliyopita mafunzo yangu ndani ya Freemason yaniwezesha kupata shahada nyingi za ngazi na umuhimu unaozidiana, ukiacha ukuu wa Wilaya nzima ya Afrika Mashariki, yaani Kenya  Sheli Sheli, Tanzania na Uganda, kwa miaka 19. Nikitaja nafasi chache tu nilizoshika, nimekuwa msimamizi wa kwanza mdogo kasha mkubwa wa kambi kuu ya viongozi wa Freemasons wa Uingereza na Wiles.

Mara ya kwanza kabisa nafasi hiyo kushikwa na mtu asiye mkazi wa Uingereza. Nimepewa heshima ya kuwa mstahiki kamanda wa kambi ya  Donyo sabuki ya royal Ark Mariner na nimeshika uongozi wa kambi hiyo toka mwaka 1990.


Mimi ni msimamizi mkuu wa Afrika mashariki wa kikosi kikuu cha Freemason cha Royal Ark cha Uingereza, nikiwa nimeshika nafasi hiyo tangu mwaka 1980, na ofisi ya wilaya tangu mwaka 1972. Mwaka 2000 nikawa Naibu Mshika upanga mkuu wa kikosi kikuu, nab ado mimi ni mkufunzi mkuu wa heshma katika kikosi kikuu cha Uskochi.

Mwaka 1987 nilipata shahada ya Mtakatifu Lawrence, shahidi; Shada ya shujaa wa Constantinople hati takatifu ya Kuhani Mkuu na Wawekezaji wakuu wa Suleiman; nikapata vilevile hati muhimu ya ushujaa ya msalaba mwekundu wa babeli mwaka 1988, nikaingia katika halmashauri ya wasimazimi wakuu namba 1, walioteuliwa na waliokuwa hodari mno nchini Uingereza na Wales, na nikapewa shahada ya  msimamizi bora kuliko wengine wote.  Mwakauliofuata nikaingia kama mwanafunzi wa mkataba katika jamii ya waabudu wa Freemasons, tawi la Row Assemblege”.

Katika maelezo ya Sir Chande hapo juu kama yaliyonukuliwa  katika kitabu chake hicho chenye kuheshimiwa sana nchini napengine hata duniani, yapo mambo mawili yenye kuhitaji udadavuzi makini zaidi. Mambo hayo ni mafunzo ya matambiko na jamii ya waabudu wa Freemasons.

Hata hivyo katika maelezo ya awali Sir Chande anasema chama hicho sio dini na wala hakiingilii dini ya mtu, wala hakimkatazi mwanachama wake kuabudu dini nyingine.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa chapisho la Kiswahili la kitabu hicho lilizinduliwa katika hafla kubwa iliyohudhuriwa na viongozi wakuu wan chi marais wastafu, mabalozi na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Shaaban Robert, Agosti 10, mwaka 2007.

Maneno yaliyopo kwenye hotuba ya Rais kikwete wakati wa uzinduzi wa kitabu hiki yanadhihirisha upekee na umuhimu wake na hata kile kilichomo ambacho wengi hawakijui. Rais katika sehemu ya hotuba hiyo alisema:

“….Aidha, napenda kukupongeza kwa dhati kwa kitendo chako cha kuandika kitabu hiki kinachohusu maisha yako. Sote  tunatambua kuwa kuandika kitabu sio kazi rahisi hata kidogo. Ni jambo linalohitaji ujasiri, umakini, nidhamu na uwezo wa hali ya juu.  Hivyo kwa  kuandika kitabu hiki  kinachogusia maisha yako kwa kipindi kinachozidi miaka 77 umeonyesha wazi kipaji na uwezo mkubwa ulio nao. Si watu wengi walio na uwezo kama ulionao wewe. Tunakupongeza sana.

Lakini kubwa zaidi nakupongeza kwa kuandika kitabu hiki kwa umakini na ufasaha mkubwa. Umeweza kwa kiwango cha hali ya juu kueleza mazingira halisi ya hali ya nchi yetu ulimokulia,  kufanyia kazi na sasa unamozeekea. Kitabu chako ni mchango mkubwa kwa historia ya nchi yetu ambayo tunauenzi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Nawaomba watanzania wenzangu wakisome kitabu hiki kila watakapopata nafasi, ninahakika watafaidika sana na kile watakachokisoma. Ingekuwa  jambo jema sana maktaba za shule na vyuo vyetu vikawa na nakala ya kitabu hiki, hivyo kuwawezesha vijana wetu kufahamu kwa undani zaidi historia ya nchi yetu na watu wake kwa ujumla”


Rais Kikwete akiwa na Sir Andy Chande

Lakini hofu kubwa kwa jamii  isiyofahamu vyema mambo hayo ni kuwepo kwa neno kuabudu ambalo tafsiri rahisi ni Tafsiri hahisi ya Neno Matambiko lililopo katika maelezo binafsi ya Sir Chande. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu ni: Utekelezaji wa ada maalumu ili kutuliza mizimu, au pepo, edah, kafara, mviga mviko.

Tafsiri ya Neno kuabudu ni: “kufanya ibada, kuheshimu kwa hali ya juu unyenyekevu wa hali ya ju. Aidha tafsiri nyingine zaidi ni tendo linaloambatana na  kutoa sadaka.

Akieleza safari yake jinsi alivyojiunga na kundi hilo Sir Chande alisema.

“Nilipoanza kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambu kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira ambayo sikuwa nayajua, ya kujitenga na dunia. Maana ingawa mpaka wakati huo Chama cha Freemason kilikuwa katika sura hiyo hiyo kwa karibu miaka mia  tatu (Kambi hizo mbili ziliunganishwa uingereza mwaka 1715), hali ya usirisiri wake unaokigubika imeongezeka sana katika miaka hii michache.

Freemason walikuwako katika sehemu yangu hii ya dunia kwa muda wa miaka hamsini, kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ikiwa imeanzishwa Zanzibar mwaka 1904, lakini ikichukua miaka mingine ishirini na minne kwa kambi ya kwanza ambayo, kwa shamra nyingi, Gavana ndiye aliyeiwekea jiwe la msingi ili ijengwe huko Bara katika Mtaa ulioitwa wakati ule; Main Avenue, sasa hivi Sokoine.

Itaendelea Jumatano Ijayo

Source: Jibu la Maisha, Jamii Forum

4 comments:

 1. KITABU HICHO KIMENFANYA KUPOTEZA IMANI NA SERIKALI.

  ReplyDelete
 2. mmmmmhh sir chande ni jasiri haogopi kutengwa na jamii

  ReplyDelete
 3. kumbe kuna watu wana ifaham tutoen gizani jaman
  kwan kama kuna vitabu bs tusome sio kila mtu kuongea
  lake mwisho tupotee miruzi mingi humpoteza ngombe

  ReplyDelete
 4. sio jambo la ajabu freemason ni uchawi kama uchawi mwingine tuu so kama mkristo unatakiwausishtuke sana coz tumepewa mamlaka yakukanyaga ng'e na nyoka...

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...