Thursday, January 26, 2012

Wananchi nchini Nigeria wamlaumu Rais Jonathan kwa ukimya wake dhidi ya Mashambulio dhidi wakristo


Askari wa Kundi la Boko Haram
Wakati Mashambulio ya magaidi nchini Nigeria yakiendelea  dhidi ya wakristo nchini humo,wanachi wan chi hiyo wamekuwa wakilaumu kila kukicha utawala wa serikali ya nchi hiyo iliyo chini ya Rais Goodluck Jonathan kwa kutochukua hatua za kutosha kuikomesha hali hiyo inayodaiwa kuendeshwa na magaidi wa kundi la Boko Haram.


Rais Jonathan ambaye ni mkristo na jina lake la kati anaitwa Ebelechukwu likimaanisha “Rehema za Mungu” amesema inawezekana kuna viongozi wa serikali yake ambao wanatumika kupeleka habari katika kundi la Boko Haram ambalo kwa muda sasa limekuwa likidaiwa kufanya mashambulio katika makanisa pamoja na ofisi za serikali. Kwa mujibu wa CNN wananchi kwa hasira wamekuwa wakitembea barabarani wakiwa mamebeba mabango na majeneza ya kebehi yakiwa na maneno yasemayo President Badluck.

Wananchi wamekuwa wakihoji kwa nini mashambulio hayo yanazidi kutokewa pasipo viongozi wa juu wa ulinzi nchini humo wakiwa hawajawajibishwa. Mashambulio hayo yanadaiwa kusababisha  kuyumba kwa umoja wa raia wa nchi hiyo. 

Mch Ayo Oritsejafor
Mch Ayo Oritsejafor ni Raisi wa chama cha wakristo nchini Nigeria (Christian Association of Nigeria's CAN),Mch Ayo amesema serikali imeshindwa kufanya maamuzi ya msingi kunusuru maisha ya wakristo. Aidha mch Ayo amesema viongozi wa Ulinzi nchini humo wamekuwa wakiwapa taarifa Boko Haram hivyo inakuwa ni ngumu kudhibiti mashambulio hayo kwa kuwa baadhi ya viongozi wa ulinzi nchini humo wameweka mbele na kuthamini udini kuliko utaifa.

Wiki iliyopita bomu moja lililodaiwa kulipuliwa na kundi la Boko haram lilipoteza uhai wa  jumla ya raia 150 katika jiji la kano nchini humo. Rais Jonathan ambaye amekuwa akitumia ukurasa wake wa facebook kutoa maoni yake kwa muda sasa amekuwa kimya huku watu wengi wakimuandikia comments za lawama kwa kutochukua hatua kali dhidi ya mashambulio hayo kwa wakristo.

Source: Christian post

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...